Rapper anaeunda kundi la Maybach Music Group Rick Ross yupo matatani kupelekwa tena mahakamani lakini time hii kwa kesi nyingine tofauti, kesi ya ubakaji!
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ Marekani, Rick Ross na rafiki yake Thaddeus “Black” James wanashtakiwa na mwanamke asiejulikana jina kwa ubakaji… mwanamke huyo anadai kuwa alialikwa na rapper huyo pamoja na rafiki yake kwenye party Los Angelesiliyokuwa inafanyika kwenye hoteli moja yenye jina W Hotel.
Kutokana na maelezo ya mtandao wa TMZ, Rick Ross na mwenzake walimfuata mwanamke huyo na gari kuelekea kwenye party hiyo… alivyokuwa kwenye gari hilo Rick Ross akamualika glasi ya kinywaji, alipojaribu kukataa baadhi ya marafiki zake Rick waliokuwa kwenye gari hilo walimlazimisha kunywa kinywaji hicho.
Baada ya kunywa glasi hiyo mwanamke huyo hakukaa muda akapoteza fahamu, alipozinduka akapewa glasi nyingine ya kinywaji, hakukaa sana akapoteza fahamu tena kwa mara ya pili, alipoaamka kesho yake aliona michubuko sehemu zake za siri zikiashiria mtu alimwingilia kwa nguvu!
Kuwauliza marafiki zake Rick Ross wakadai hawajui kilichotokea kati yake na rafiki yake Rick Ross “Black James” ila walikuwa wote pamoja na rapper huyo!.. TMZ wanasema Mwanamke huyo ameamua kupeleka mashtaka yake polisi huku akimtaja Rick Rosskama mtu alietengeneza mchongo huo, inasemekana pia gari lililotumika kwenda kwenye hiyo party ni la Rick Ross.
No comments:
Post a Comment