Kama vile ilivyo brand ya movie ya Bad Boys, movie za Men In Black haziwezi kuongelewa bila kumtaja staa wake Will Smith na kama ulikuwa hujui basi taarifa ikufikie kuwa part 4 ya movie hiyo iko njiani mtu wangu lakini bad news ni kwamba Will Smith hatokuepo kwenye movie hiyo safari hii, kwa nini!? iko hivi…
Watengenezaji wa movie hiyo Walter Parkes na mwenzake Laurie MacDonald walipata time ya kukaa na kuongea na mtandao wa The Hollywood Reporter wa Marekani na kueleza kwanini wameamua kutokumuweka Will Smith kwenye movie hiyo safari hii..
>>> “Tunatengeneza
kama series ya muendelezo wa movie iliyopita, tutaibadilisha kidogo na
pengine Will Smith hatoonekana kwenye muendelezo wa movie ya safari hii…
tuna mtazamo tofauti safari hii wa jinsi tunavyotaka kuipeleka brand ya
Men In Black, Will Smith amefanya kazi nzuri sana kwa movie zilizopita
ila safari hii tumesukumwa kufanya vitu tofauti kidogo…” <<< @Laurie MacDonald.
Movie za Men In Black zimemuingizia Will Smith hela
ndefu sana kwa miaka yote aliyokuwa anazicheza na licha ya yeye
kutokuepo kwenye movie hiyo time hii, mwigizaji huyo ameungana na rapper Jay Z na pamoja wanategemea kutengeneza mini series itakayo onyeshwa HBO hivi karibuni.
Will Smith na kampuni yake ya Overbrook Entertainment pia wana mpango wa kutengeneza movie itakayofana na series ya ‘The Fresh Prince of Bel-Air’, series iliyompatia umaarufu mkubwa sana Will Smith miaka ya 90.
No comments:
Post a Comment