Kama wewe ni mpenzi wa Movie najua utakumbuka movie kali ya 12 Years A Slave ambayo ilitoka mwaka 2013 na ndani yake kulikuwa na mastaa kibao wakali ikiwemo Michael Fassbender, Chiwetel Ejiofor na Brad Pitt. .. Lakini yuko mrembo toka Kenya pia, Lupita Nyong’o…
movie hiyo ilikuwa njia ya kumsogeza mrembo huyo kufahamika Duniani
kote na baadae akaanza kupata madili kibao ikiwemo ya Fashion na
biashara nyingine.
Lupita alitua
nyumbani kwao Kenya na hata alipoondoka hakukosa story za kusimulia
kuhusu mambo ya Kenya… Lupita anasimulia hii kuhusu kuolewa >>>
“Nilipokuwa Kenya kuna siku nilikuwa
kwenye gari na mama yangu, akasema ‘ile ni shule nzuri sana kwa watoto’,
alafu akageuka kuniangalia… Mama anataka niwe na watoto kwa sasa“– Lupita Nyong’o.
Okay, baada ya hilo kuna hiki alikitolea
jibu pia, je ataolewa nyumbani kwao Kenya na watoto wake atawalea Kenya
pia? >>> “Itategemeana na wakati wenyewe itakavyokuwa akipatikana mwanaume wa kunioa“- Lupita.
No comments:
Post a Comment