Unaamini katika bahati,? katika jamii zetu kuna ishara nyingi
Baadhi ya watu huwa wanaamini kama ni ishara ya bahati nzuri (Lucky)
kucheza kwa jicho la kulia kwa juu wapo watu wanao amini ni ishara ya
kupata zawadi,kupata ujumbe mzuri ama jambo lolote ile zuri, hata mimi
huamini hivyo, na wapo wanao amini kuwashwa kwa mkono wa kulia ni
ishara ya kupokea pesa wengi tumemekua tukiamini hivyo na wengine
huwaomba watu wao wa karibu wawaandikie kiasi cha pesa kwenye mikono
yao. Kama utabiri wa kupokea pesa hiyo.
Ila mambo haya ya kuamini katika bahati yapo katika jamii zingine pia
ambazo sio za kiafrika na wao pia wana vitu ambavyo wanaamini wakiviona
ni ishara ya bahati kwao.
Kobe
Kwa jamii ya wachina ukikutana na kobe ni ishara nzuri ya mambo
mazuri, wao wanaamini ni nyota njema kwao na ishara ya maisha marefu au
kufanikiwa.
Nyota (Falling Star)
Wengi tuna tabia ya kuita kimondo, ila kwa wengine wanaita falling
star, kuona kama nyota inaanguka inapita kama moto na kupotelea angani,
kwa jamii zingine wanaamini kama unataka kuomba kitu na ukaiona nyota
ile basi ni wakati mzuri wa kuomba kitu icho (Make a wish) na unaomba
wakati unaiona hiyo nyota kabla haijaishia na kwa imani yao ni lazima
kitatokea kitu kile ulichoomba.
Tembo
Kwa baadhi ya jamii ya wahindi wanaamini ukiwa safarini na ukawaona
tembo basi safari yako iko salama na utafika kwa usalama, na tembo pia
wanaashiria madaraka, nguvu, utulivu, na ukarimu
Upinde wa Mvua (Rainbow)
Sijui kwa jamii za wengine ila wengi wanaamini ni ishara ya kutokuwa
na mvua tena baada ya kuona upinde wa mvua lakini kwa jamii zingine kwao
ni kama bahati. Wanaamini kuna kitu kizuri kitatokea mbeleni ama ishara
ya mafanikio.
Namba Saba
Kwa jamii ya wajapani number saba inasimamia miungu saba ya bahati,
wakati kwa wengine wanaamini number saba inasimama kama zawadi saba
kutoka kwa Mungu ambazo ni busara, nguvu, uelewa,Baraka, heshima,neema
na uwepo wa nguvu ya Mungu katika maisha yako, wao wanaamini katika
number saba kwahiyo kwao ukizaliwa tarehe saba ama ukafanya dili la pesa
siku ya tarehe hiyo ni bahati kwako na utafanikiwa
Dolpin (Pomboo)
Aina hii ya samaki kwa jamii ya watu wa Amerika ni ishara ya bahati
kwao kama wavuvi wakiwaona samaki hawa ni shara ya kuwa na samaki wengi
mbele yaani watavua samaki wengi vile vile ni shara ya kuwa na kisiwa
karibu au wapo karibu na nchi kavu, na samaki hawa huwa hawaliwi kwa
sababu ya heshima hiyo.
No comments:
Post a Comment