Jipangie Bajeti na Mpango wa kifedha
Ili uendelee lazima ujue, unatumia nini unaingiza nini? hii
itakusaidia pia katika akiba zako na itakusaidia kama utachukulia swala
hilo kwa umakini, kama kuna bili za kulipa kila mwezi na lazima uziweke
katika mtiririko mzuri wa malipo ili bajeti zako siziingiliane na akiba
zako wala matumizi yako binafsi.
Uwe na Vyazo Vingine Vya Kukuingizia Kipato
Hakikisha mshahara wako sio pesa pekee unayoitegemea, lazima
utengeneza mifereji mingine ya kukuingizia kipato, fanya kazi mwenyewe
kama bosi wa biashara yako au ofisi yako, uza bidhaa zako kwa mitandao
ya kijamii, anza kujitangaza taratibu sio lazima uanze na mtaji mkubwa.
ukiwa na vyanzo vingi vya mapato ni rahisi kuweka akiba na kuwekeza.
Akiba,Akiba, Akiba weka Akiba
Watu walioendelea waliweka akiba, punguza vitu unavyofanya visivyo
vya maana au visivyo na umuhimu, punguza kutoka sana na kutumia pesa kwa
starehe, fanya mambo ya muhimu tu acha kununua vitu ambavyo
hauvihitaji, anza kwa kuweka akiba ndogo, ukiweka akiba nyingi ndiyo
utaweza kuwekeza zaidi. wasichana wengi wanatabia ya kununua vitu
wasivyo vihitaji kama viatu vingi,Nguo,Mikoba na vifaa vya Urembo.
Jiwekee kiwango cha wastani kulingana na mahitaji yako.
Punguza Matumizi
Watu wengi wakipata pesa kidogo wanakimbilia magari ya bei kubwa na
kufanya manunuzi ya vitu vya gharama kama nguo,saa na viatu kwenye
maduka maarufu mjini, lakini kama ungetumia pesa kuwekeza katika mambo
ya muhimu kama biashara lazima baadae ikulipe kuna usemi mmoja unasema
“Buy the best Car but Own the Best House” na usinunue kitu ambacho
haukihitaji sababu tu ni bei rahisi,
Kutana na Watu wenye Utaalamu
Kutana na watu walio kuzidi ujuzi,utaalamu na Uzoefu katika Biashara au
shughuli unayotaka kuifanya hii itakusaidia kujifunza vitu kutoka kwao
tembelea mikutano mbalimbali ya wataalamu na masomo mbalimbali ya muda
mfupi kujiongezea utaalamu, jiunge na wafanya biashara au wajasiriamali
walio endelea katika kujifunza mambo ya kuhifadhi fedha, kuweka akiba na
kuwekeza katika biashara.
No comments:
Post a Comment