Tukiwa na Siku chache kumaliza Mwaka, ni wakati wa kuangalia nini
umefanya ndani ya mwaka mzima, nini umeingiza nini umepoteza ulipanga
ndoa imefanikiwa? Ulipanga biashara imefanikiwa? na vingine vingi
lakini wakati unaangalia nini umepata nini umejifunza ni wakati pia wa
kuangalia mbele, zimebaki siku chache mwaka uishe una mipango gani na
mwaka mpya, kuna vitu vinaweza kuwa muhimu kwako au kwa mwengine lakini
nadhani kila mtu anatakiwa kuzingati kabla hajaanza mwaka mpya.
Jaribu Mambo Mapya/ Kubali Mabadiliko
Umefanya kitu kimoja kwa mwaka na zaidi na hauoni mafanikio badilika,
jaribu kujifunza mambo mapya, fanya mabadiliko juu ya mtazamo wako juu
ya maisha,biashara,mahusiano,elimu na mengine mengi, unatembelea sehemu
hizo hizo kila siku, filamu hizo hizo, marafiki hao hao, ni wakati wa
kukutana na watu wapya na ujifunze mambo tofauti hii itakuza uwezo wako
wa kufikiri.
Kazi, kazi, Kazi
Nimerudia kuonyesha msisitizo, fanya kazi, ulichokifanya jana
kukufikisha hapo ulipo leo,hakiwezi kukufikisha unakoenda kesho
unahitaji kazi zaidi kufika unakoenda kesho, ongeza juhudi katika kazi
zako, kama ni masomo ongeza juhudi pia, unahitaji kujishughulisha
kuendelea maendeleo hayaji kwa kukaa na kula bata kila siku, badilika.
Umejifunza Nini kutokana na Makosa yako
Umeshindwa kufikisha malengo uliyoweka mwaka jana juu ya mwaka huu je
unadhani malengo hayo yatafanikiwa mwaka unaokuja. Unajua ulikosea
wapi? Unajua wapi unatakiwa kuanzia ni wakati wako wa kijibu maswali
hayo, na ni wakati wa kuangalia nini kilisababisha ukashindwa
kufanikisha malengo yako. Na unatakiwa kufanya nini kukabiliana na
changamoto hizo ni wakati wa kujifunza kutokana na makosa yako.
Karibisha Mawazo Chanya/ Yaliyopita Yamepita
Toa mawazo finyu juu ya maendeleo yako, karibisha mawazo mapya katika
kila jambo, na uyaache mambo ya nyuma yapite na uwe tayari kukutana na
mambo mengine mbele yako, huwezi badilisha historia lakini unaweza
kutengeneza mambo ya mbele yako.
Usifanyiwe Maamuzi na Mtu
Kuna watu bado kila anachotaka kufanya anahitaji aambiwe na mtu,
mpenzi au mzazi hatukatai wazazi muhimu ila kuwa na maamuzi yako
binafsi,ndugu, marafiki na jamaa wana umuhimu kwako, cha muhimu ni kujua
nini unataka kufanya na ufanye kwa moyo. Jaribu kujiamulia na uwe
nahodha wa maisha yako mwenyewe. Jua wakati gani wa kusema ndio na
wakati gani wa kusema hapana
Kuna Tabia za Kuacha
Kuna baadhi ya tabia ambazo zinakukwamisha, ni muhimu ukaziacha kama,
ulevi ya kupindukia, uhuni, matumizi ya sigara na mengine mengi ,
jijengee tabia za maendeleo kutana na watu wapya, soma vitabu, tembelea
sehemu hujawahi kwenda, jifunze lugha mpya, jifunze kucheza ala yoyote
ya mziki. Tabia chanya ni chachu ya maendeleo.
World Of Pl@tnumz
Lifestyle
Umetimiza malengo yako ya mwaka 2015 ? Haya ni mambo ya kuzingatia ili uweze kufanikisha ya mwaka ujao.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment