Msongo wa Mawazo au Stress kama wengi walivyozoea ni kitu kinampata
kila mtu, na wakati mwingine hujui kama unastress, wapo wanaodhani mtu
akiwa na stress lazima awe kama kachanganyikiwa ama analia hivi na vitu
kama hivyo, wapo walio na stress na huwezi wajua na unaweza ukawa na
stress usijue ukadhani ni hali yako ya mwili kawaida ila kama una
dalili zifwatazo kuna uwezekano unasumbuliwa na msongo wa mawazo na
haujui.
Maumivu ya kichwa ya Mara kwa Mara
Kama haujafanya kazi ngumu, unakunywa maji vizuri, hauna malaria wala
ugonjwa wowote,hufanyi kazi juani na unapata maumivu ya kichwa mara kwa
mara, hizo zinaweza kuwa stress, unatakiwa kukaa chini na kujaribu
kutafuta ni mambo au kitu gani kinakupa hizo stress na ujue jinsi ya
kujitoa katika msongo huo wa mawazo. Maumivu yakizidi unashauriwa
kumuona daktari
Mzio au Allergies
Sio kila wakati chakula Fulani Fulani, hakikupendi au mafuta Fulani
unayotumia katika ngozi yako hayakupendi, si wakati wote, mzio
unahusisha mazingira yako yanayokuzunguka wakati mwingine ni sababu ya
stess ulizonazo, na wakati wa kukutana na wataalamu (specialist) ambazo
wanaweza kukusaidia tatizo lako kwa undani.
Kujihisi Mgonjwa Mgonjwa Wakati wote
Unapokuwa unajihisi homa za mara kwa mara, kuchoka sana wakati
mwingine, inaweza kuwa ni dalili za msongo wa mawazo na sio tu kuwa na
afya mbovu lakini pia stress zinaweza chelewesha uponaji wa kidonda
chochote mwilini kama uliumia, na hii inaweza sababisha maradhi
mengine kwenye kidonda chako,(infections)
Huwezi kufikiria sawasawa
Unashindwa kuwaza vitu kwa umakini na kuvichanganua kwa wakati, kila
kitu kinaonekana kizito hata kama ni kitu kidogo kukitafakari lakini
utachukua muda kuwaza na kuwazua hii pia ni dalili ya kuwa na msongo wa
mawazo (Stress) na hii huambatana na tatizo la kusahau sahau mambo.
Unakosa Usingizi
Kuna watu wanatumia pombe ili walale na kuna wakati wanadhani ni
kawaida tu hawawezi kulala kama hawajatumia pombe, lakini kama unapata
tatizo la usingizi hiyo pia ni dalili kubwa za msongo wa mawazo cha
msingi ni kupunguza vinywaji vilivyo na kafaini na kufanya sana mazoezi
hiyo inaweza kuufanya mwili uka relax ukapumzika vizuri lakini pia
unaweza kumuona dakatri kwa ushauri zaidi juu ya afya yako.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment