Ukitaka kujua uhondo wa ngoma sharti uingie ndani ucheze si ndio,
kuna mambo ya kuwahusu wanaume huwezi yasikia kwa wanaume wenyewe lakini
ukikaa na wanawake wanaweza kukwambia ni makosa gani wanaume
wanayafanya hasa wakiwa faragha,ambayo hayawapendezi na wanaume wengi
huwa hawajui kama hayo ni makosa .
Kuandaa Mazingira
Mazingira, naongelea muonekano mzima, wa eneo la tukio lazima kuwe
kusafi, sio nguo chafu ziko kila sehemu, sebuleni umeweka makopo ya soda
yameisha vipande vya mkate, viatu vya matope ilimradi shida, lakini
wengi wanashindwa kuandaa mazingira, weka nyumba yako safi, manukato,
mziki mzuri weka mwanga mdogo au la washa mishumaa,kuweka mazingira
yavutie kabla ya game.
Maandalizi
Kwa mwanamke yeyote, maandalizi ya mwanzo kabla ya show nzima ni
muhimu sana, ila wanaume wengi wanaharaka ya kumaliza mchezo, hata
wachezaji mpira wanafanya kwanza warm up kabla ya kuingia uwanjani
unadhani kwanini? Kwahiyo cha muhimu ni kukumbuka jinsi ya kumpa mwenza
wako maandalizi ya kutosha yanahitajika sana.
Kuwa na Papara
Kuna watu wana papara, unashindwa kufanya maandalizi ya awali na bado
unaharaka kama mwana riadha, sio adhabu wala sio ugomvi wanawake
wanapenda kulelewa, nenda nae taratibu muachie muda wa kupumua, sikiliza
mapigo yake ya moyo, muongeleshe taratibu, alafu uendelee .
Kutokujua Kusoma Mchezo
Wanawake wengi wana aibu ya kusema nini wanataka wakiwa kitandani,
ila kuwa mjanja na usome alama za nyakati wanaume wengi wanafeli hapo,
kuna wakati wa kuongea kama mabubu, ni wewe tu kujua nini maana
yake,usisubiri uambiwe, kwahiyo kuna wakati unashindwa kumpa mpenzi wako
huduma anayoitaka sababu hukuweza kumsoma nini anataka.
Unataka kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja
Sio kila staili uliyoiona unataka kugeza siku moja, kuwa mstaarabu na
jaribu kila moja kwa wakati, haina haya ya kufanya zote kwa siku moja,
na mambo mengine pia sio ya kugeza, mnaweza kuongea kabla ya kuanza kitu
kipya kama na mwenza wako yupo tayari kwa hilo, usilazimishe.
Ingependeza kama mtafanya vitu kila mtu anafurahia na mtakuwa huru
kufanya mambo yenu kwa amani.
Kumvunjia heshima mwenza wako
Kuna baadhi ya vitu si kila mwanamke anapenda kufanyiwa,kama kumuita
majina ya ajabu ajabu uliyo ona katika filamu Fulani au video za ngono,
usifanye mambo hayo wengine hawajisikii vizuri kufananishwa na wale
wanawake wa kwenye video za ngono, baadhi ya wanawake huchukulia swala
hili kama kumvunjia heshima, na wapo wanaume wanafanya michezo hii.
Kitu ambacho kiukweli hakipendezi.
Usijifanye Wewe ndio Kiongozi
Wapo wanaume wanapenda kuwa viongozi kila sehemu lakini sio kitandani
bwana, mnatakiwa kuwa na ushirikiano,sio kila kitu unataka kwa
kulazimisha, kuwa mtaratibu na mstaarabu na unaweza ukamuacha mpenzi
wako afanye anachotaka kufanya na wewe bila wewe kutoa maelekezo.
Kusahau Sehemu Muhimu
Kila mtu ana sehemu za kumfanya apate mzuka zaidi wapo wanaume
wanasahau haya, wao wanajua kuwahi tu sehemu wanayoitaka wakiwa
kitandani ni kosa, jua kucheza na mwili wa mwenza wako,lazima ujue ni
wapi mpenzi wako anapenda kushikwa ama kutomaswa wakati wa faragha
Kuhisi Karidhika
Usijidai kwamba wewe unajua kutoa show kali basi lazima atakuwa
amefurahia, muulize kama ameridhika, wanaume wengi hawaulizi ili, ni
kosa unaweza ukawa hata hujampa kile alichokuwa anataka na kwa sababu
wanawake wengi sio watu wa kuweka mambo wazi hatoweza kukueleza kuhusu
alivyojisikia. Ila anaweza sema kama ukiuliza.
Kumfanya kiburudisho
Kuna baadhi ya wanaume wanawafanya wanawake zao kama kiburudisho
akimaliza haja zake anavaa na kuondoka, au ndo akimaliza atageukia
upande wa pili na usingizi juu, tafadhari sio mchezo mzuri kufanya hayo
kwa mwenza wako, inapendeza kama mtaongea hata kwa nusu saa baada ya
kumaliza kabla ya kila mtu kufanya yake.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment