Tomboy ni nani? Tomboy ni mwanamke anaependa sana mambo ya kiume,
wengine wanawaita majike dume, kitu kimoja ambacho wanaume wengi hawajui
sio kila mwanamke anaependa kujitupia pamba za kiume au anapenda
kufanya mambo Fulani ya kiume ni msagaji. Wapo ambao wameamua kufanya
hiyo staili yao ya maisha, wapo ambao wanajiona wabaya na wanadhani
hawawezi kupendwa na mwanaume yoyote, wapo ambao waliumizwa kwenye
mapenzi na wanajaribu kujiweka kiume ili wasipate tena wapenzi.
Hawa mnaowaita madume jike pia ni wanawake na wanahisia kama wanawake
wengine, wanapenda kama wanawake wengine ila kwa sababu wanajiweka kama
wanaume inakuwa vigumu kumtamkia mwanamme kama wanampenda na
kutokujiamini, wengine wanajiona sio wanawake kamili. Na nina amini
wanaume wanamchango mkubwa kuwabadilisha wanawake wa aina hii kuwa kama
wanawake wengine bila kutumia nguvu. Kuna faida kadhaa kutoka na
mwanamke wa aina hii.
Sio Mwanamke wa kioo kila mara:
Wanawake wa aina hii hawapendi kujiremba sana, kwahiyo hutoboreka
wakati wa kutoka nae akipiga tshirt na jeans maisha yanaenda,
hatokusumbua kutengeneza nywele wengi wao wanapenda kukata nywele au
kuweka dreads hautokuwa na gharama za kumpeleka saluni.Sio wanawake wa
kubandika kucha wala kope wanaweka kila kitu simple.
Hutomkuta kwenye Vigenge vya Umbea:
Wanawake wa aina hii huwa hawana marafiki wengi wa kike, hawapendi
umbea umbea na kupiga soga kijinga, kwahiyo hawezi kuwa na mashoga wa
kijinga wanao shauriana ujinga na mambo yasiyo ya maana.
Waaminifu:
Sio wanawake wanaofwatwa na wanaume wengi,kwahiyo mwanaume ambae
atajitokeza kwake na kumpenda huwa anampa mapenzi yake yote na kama
unajua mapenzi na kumjali na kumuonyesha mapenzi ya dhati kabisa basi
utashangaa,wanawake wa aina hii ni wepesi kubadilika na kuwa kama
wanawake wengine watavaa nguo za kike na kuwa kama wanawake wengine ili
uzidi kuvutiwa nao.
Mtafanya Mambo mengi pamoja:
kwa kuwa anapenda mambo mengi ya kiume mtajikuta mnaangalia mpira
pamoja mnacheza game za Tv pamoja na kunywa mkitoka pamoja na washikaji
na hii itawafanya muwe wapenzi ambao pia ni marafiki, kitu ambacho
wapenzi wengi hawana. Kuwa na mpenzi ambae pia unaweza kumchukulia kama
rafiki ni kitu kinachowafanya wapenzi muwe kama mapacha inaongeza
chachu ya mapenzi yenu.
Hawana Drama za kijinga:
Wanawake wa aina hii, hawapendi drama nadhani mnawajua Drama Queen
hao ni wanawake wanapenda kufeki mambo, kitu kidogo wanajidai kupanick,
kujizimisha na kujitia presha lakini Tomboy ukifanya kitu atakuambia na
hawajui kuigiza wako real, na ni wanawake waelewa kuliko wanawake
wengine wanaojivalia kidada.
World Of Pl@tnumz
Lifestyle
Unafahamu faida za kuwa na uhusiano na wasichana wenye tabia za kiume(Tomboy)?
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment