Zile habari za nakupenda, nakupenda pia kila mtu anajua siku hizi na
ni kawaida kwa miaka ya sasa, kuitana baby, hubby,sweet,mpenzi,
mahabuba na majina mengine mengi sio lazima niyataje yote, ila unajua
huyo mahabuba wako hata kama anakupenda vipi kuna vitu hawezi kukwambia
ukweli, kuna vitu katika mahusiano watu huwa wanafichana na hata kama
mnaambiana basi mnadanganyana.
Mahusiano yako ya nyuma
Ni vigumu sana wapenzi kuelezana historia zao za mapenzi hasa
inapokuja swala la umetembea na wangapi? Hapa kama uliambiwa
umedanganywa tafiti zinaonyesha wanaume ndo wanajua kudanganya kwenye
swala hili kuliko wanawake japokuwa kwa asilimia kubwa wapenzi huwa
hawaambiani ukweli kuhusu watu wangapi wameshakuwa na mahusiano nao ya
kimapenzi. Kwahiyo ni bora usiulize usijisumbue.
Kipato
Hapa inakuwa shida kidogo kwani hela haina mapenzi, haina undugu na
ni mara chache ukute wapenzi wanajua mishahara au kipato cha mwenza
wake, wapenzi wengi huwa wanafichana na wengine hata wanadanganya kuhusu
madeni waliyonayo ni kawaida sana kwa mapenzi ya sasa hasa hali ya
kipato ilivyo ngumu.
Kufurahia Tendo
Wapenzi wengi hawaambiani kweli hasa wanapo kutana kimwili, kama
walifurahia au walichukia, wanawake wanasifika kwa kudanganya
wameridhika, ila pia wanaume huwa hawasemi kama msichana hayuko vizuri
kwenye game, na ndo maana watu baada ya kuachana ndo utasikia
wanachafuana oooh wewe ulikuwa kama gogo na mara ooh wewe ulikuwa kama
toothpick mambo kama hayo.
Muonekano
Kuna wakati mtu anapoteza mvuto wake wa asili lakini inakuwa vigumu
kwa wapenzi kuambiana ukweli labda mtu amenenepa sana, au amekuwa na
kitambi sana na hana mvuto lakini sababu ya mapenzi au uoga inakuwa
vigumu wapenzi hawa kuambiana ukweli
Matumizi ya Kilevi
Kwenye matumizi ya pombe baadhi huwa wanakuwa wawazi, lakini wapo
wanaoficha matumizi mengine ya kilevi kama kuvuta sigara na matumizi ya
miraa au mirungi,
Hisia zake kwa mpenzi wa zamani (EX)
Wapo watu wanaingia kwenye mahusiano wakiwa bado wana hisia za
mapenzi na wapenzi wao wa zamani lakini sio rahisi kusema hayo kwa
wapenzi wao,na hata wakiulizwa huwa wanadanganya. Na sio raisi kuleta
habari za mapenzi ya nyuma kwa mpenzi mpya. Ni vigumu kukwambia
anavyojisikia jua ya mpenzi wake wa zamani.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment