Wiki iliyopita taarifa za kuvamiwa kwa nyumba ya Big Sean iliyopo Los
Angeles, Marekani wakati akiwa mapumzikoni Dubai zilienea mtandaoni
ambapo wezi waliovamia nyumbani hapo waliiba vitu vyenye thamani ya
dolla 150,000 na kuondoka na nyimbo za rapper huyo ambazo hazijatoka.
Taarifa mpya zina sema wezi hao ambao wanadhaniwa kuwa watu wa karibu
na rapper huyo waliacha ujumbe wenye e-mail yao iwapo Big sean
atahitaji kurudishiwa nyimbo zake hizo.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa kesi hiyo kwasasa infatiliwa na kikosi maalumu “special unit” cha LAPD
Imeripotiwa kuwa lengo la wezi hao kuacha ujumbe huo ni kwa ajili ya
kutaka rapper huyo awalipe kiasi kikubwa cha pesa ili apate nyimbo zake
na ripoti zingine zimedai kuwa ni mpango wa wezi hao kuwachanganya
polisi kuwatafuta kupitia email hiyo isiyo ya kweli.
World Of Pl@tnumz
Entertainment
Music Stories
Waliovamia nyumbani kwa Big sean na kupora kazi zake waliacha ujumbe wenye e-mail yao kama atazihitaji tena
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment