Kuna watu wakinunua gari mpya wanaita mafanikio, wengine kununua au
kujenga nyumba kwao ni mafanikio, kila mtu anatafakari mafanikio vile
yeye anavyoelewa, mi naelewa mafanikio ni kutoka sehemu moja kwenda
nyingine kimaendeleo. Kufanikisha mambo yote ya msingi, kuwekeza na bado
umeweka Akiba. Sitoshangaa kama wewe mafanikio yako ni kununua nguo
mpya au kiatu kipya hayo yanaweza kuwa kwako mafanikio watu
tunatofautiana sana kwenye kufikiri. Ila umeshawahi kuwaza kwanini
hufanikiwi katika maisha Yako ?
Huna Malengo ya Baadae
Kuna watu hawajui ndoto zao,hawajui nini wanataka kufanya katika
maisha yao, wapo walio na ndoto za kufanya mambo kadhaa kama kuwa
wanamitindo, wanamuziki au wacheza filamu lakini hawajui wapi wanaanzia,
unatakiwa kujua unaanza wapi, kuwa kiongozi wa maisha yako mwenyewe kwa
kupanga mipango yako weka plan A na plan B na hakikisha unafanikisha,
jiekee muda (Deadline) mfano ndani ya miaka 5 au zaidi uwe umefanikisha
malengo hayo.
Una Marafiki ambayo sio mfano wa kuigwa
Unapohitaji maendeleo jaribu kuachana na marafiki ambao kazi yao
kubwa ni kukukatisha tamaa au kukurudisha nyuma kimaendeleo, kutana na
watu wenye fikra chanya (Positive People) kaa na watu ambao wana mchango
mkubwa wa maendeleo yako. Mchango sio lazima uwe pesa unaweza kuwa
mawazo au mchongo.
Muoga wa kujaribu
Kuna kukosea sana wakati wa kuaanza chochote, usiogope kujaribu tena
kama ulishindwa mara ya kwanza kila alie na mafanikio hakuanzia juu,wote
walianzia chini, fanya unachopenda na sio unachoweza kufanya. Kufanya
kazi kwa kuwa unaipenda utafanikiwa kuliko kufanya kazi sababu unaiweza.
Haukubali Makosa yako
Kubali kurekebishwa, hauwezi kuwa uko sahihi wakati wote, sote
tunakosea ila kuna wakati wa kuruhusu watu wakukosoe pale unapokosea
kwani ndo njia raisi ya mafanikio na unatakiwa kujifunza kupitia makosa
hayo kama biashara ilikufa mwanzo lazima ujue nini kilisababisha ikafa
na usije ukafanya makosa kama hayo tena.
Huweki Akiba
Kuna watu wanadhani akiba lazima uwe na mamilioni katika akaunti ya
benki lakini kama unafikiria mbele zaidi lazima uwe na akiba kwa kila
unachopata, au hata uwe umewekeza katika biashara hii itakusaidia kupata
kipato zaidi ya kimoja. Biashara sio lazima ufungue kampuni watu
wanaanzia chini. Kwenye pikipiki,Bajaj Hadi maroli ya kusafirisha
mizigo usikate tamaa.
Unatumia kuliko unachopata
Starehe gharama sana wote tunajua, kuna usemi unasema “Work Hard Play
Hard” fanya kwanza kazi kwa bidii, kuna watu wanapenda starehe hadi
wanakopa pesa za kunywa pombe wanakuwa na madeni ambayo hayana faida,
hiyo sio akili.
Unajifananisha na wengine
Kitu kimoja watu wengi hawajui Hamisi hawezi kuwa Nasibu acha tabia
ya kujifananisha na mtu na kuwaza kwanini hujawa kama yeye, yeye ana
njia zake za maisha tofauti na zako jaribu kutafuta vya kwako. Na
usijaribu pia kugeza kupitia njia zake za maendeleo kama yeye
anafanikiwa kwa kuuza viatu sio lazima na wewe uuze viatu.
World Of Pl@tnumz
Lifestyle
Haya ni mambo yanayowezakukwamisha mafanikio yako bila mwenyewe kujua...
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment