Breaking News
recent

WIZARA YA MAMBO YA NCHI ZA NJE YAFUNGUKA KUHUSU MREMBO WA KITANZANIA KUNYONGWA MISRI

Akizungumza na Gazeti la
Mwananchi jana Mkuu wa
Kitengo cha Habari cha
Wizara ya Mambo ya Nje na
Uhusiano wa Kimataifa,
Mkubwa Ali, alikiri
kukamatwa kwa watu hao
(majina yanahifadhiwa)
ambao mmoja ni mkazi wa
Ilala na mwingine wa
Magomeni jijini Dar es
Salaam. “Taarifa tulizonazo
zilizo rasmi kutoka Ubalozi
wa Tanzania nchini Misri kwa
sasa ni kukamatwa kwa
Watanzania wawili
waliokuwa wakisafirisha
heroin kuelekea Bara la Asia
na walikamatwa nchini Misri
wiki mbili zilizopita.”
“Tumewasiliana na balozi wetu
nchini Misri amesema hana
taarifa za kuhukumiwa
kunyongwa kwa watuhumiwa
hao, isipokuwa
wameshasomewa shtaka lao la
awali. Wapo rumande kwa sasa
kwani kesi hiyo imetajwa mara
moja tu. Balozi amekiri
kushikiliwa kwa watuhumiwa
hao wakiwa na dawa
zinazoaminiwa ni za kulevya,”
alisema.
Alisema watuhumiwa wote
wanashikiliwa polisi na
wanatarajia kufikishwa
mahakamani wakati wowote.
Video inayomwonyesha mmoja
akikaguliwa na maofisa wa
polisi wa nchini Misri na
kukutwa na dawa hizo,
ilisambaa siku nne zilizopita
katika mitandao mbalimbali ya
kijamii.,
Kwa mujibu wa sheria za Misri
kama ilivyo kwa nchi za Bara la
Asia, mtu akikamatwa na dawa
za kulevya hukumu yake ni
kunyongwa hadi kufa.
Kutokana na sheria za nchi
hiyo, tangu kukamatwa na
Watanzania habari zimeenea
kuwa huenda wakanyongwa.
Habari za uhakika kutoka kwa
ndugu wa karibu wa
mtuhumiwa huyo, zilidai kuwa
walikuwa hawafahamu kuwa
alikuwa anajihusisha na dawa
za kulevya.
“Huyu ni ndugu yangu kabisa
lakini nilikuwa sijui kama
anafanya mambo kama hayo’’
alisema.
kama atanyongwa ni pigo
kubwa kwetu,” alisema mmoja
wa ndugu wa Sharifa ambaye
hakupenda kutaja jina lake
Alisema miaka mitatu iliyopita
ndugu yao wa kike mwenye
mtoto mmoja alikuwa akifanya
kazi katika Shirika la Nivea na
alikuwa hana tabia mbaya.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.