Breaking News
recent

Dola milioni 7 kwa mwenye habari kuhusu Boko Haram

Marekani inaahidi kutoa zawadi ya
fedha kwa yeyote atakayetoa
habari kuhusu makundi ya
wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini
na Magharibi mwa Afrika.
Wizara ya mambo ya ndani nchini
Marekani inasema itatoa dola
milioni saba kwa yeyote
atakayetoa taarifa kuhusu aliko
kiongozi wa Boko Haram Abubakar
Shekau.
Zawadi nyingine za kima kidogo
pia zitatolewa kwa wale
watakaokuwa na habari kuhusu
viongozi wa kundi la kigaidi la Al-
Qaeda Kaskazini mwa Afrika na
wale wa kundi la (Movement for
Unity and Jihad) Afrika Magharibi.
Yeyote atakayepasha habari
kuhusu kiongozi wa zamani wa
kigaidi Mokhtar Belmokhtar
ataweza kupokea dola milioni
tano.
Kundi lake la wapiganaji
lijulikanalo kama, Blood
Battalion,linasemekana lilifanya
shambulizi dhidi ya kiwanda cha
gesi, Kusini mashariki mwa Algeria
mwezi Januari ambapo mateka 37
waliuawa wakiwemo wamarekani
watatu.
Donge nono la dola milioni tano
pia lilitolewa kwa mtu ambaye
angetoa habari kumhusu kamanda
mkuu wa wapiganaji wa kiisilamu
Yahya Abu el Hammam, ambaye
Marekani ilipanga kushambulia
watu na kuwateka nyara wageni
katika kanda ya Afrika Magharibi.
Wizara hiyo ilisema kuwa takriban
dola milioni 3 zitatolewa kwa
watakaotoa habari kuhusu
viongozi wengine wa kigaidi
wakiwemo, Malik Abou Abdelkarim
na msemaji wa kundi la (Mujao)
Oumar Ould Hamaha.
Inaarifiwa kuwa Oumar Ould
Hamaha, alihusika na visa vya
utekaji nyara wa raia wa kigeni
nchini Niger mwaka 2008 na kudai
kulipwa kabla ya kuwaachilia
Kundi la Boko Haram, limekuwa
likifanya mashambulizi makali
Kaskazini mwa Nigeria, na
kusababisha vifo vya watu 2,000
tangu mwaka 2009.
Kumekuwa na wasiwasi mkubwa
kuhusu kuwepo uhusiano kati ya
Boko Haramna makundi mengine
ya kigaidi katika nchi zingine katika
kanda hiyo ikiwemo kundi laAQIM.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.