Breaking News
recent

Vijusi wanaweza kuonyesha hisia tumboni.

Vijusi au mtoto ambaye angali
kuzaliwa akiwa bado kwenye
mfuko wa uzazi, hujifunza
kuonyesha hisia za uchungu
wakiwa bado tumboni. Hii ni kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa katika
vyo vikuu vya Durham na
Lancaster nchini Uingereza.
Wanaamini kuwa vijusi hujifunza
namna ya kuwasiliana baada ya
kuzaliwa kwa njia za kulia au kwa
kukunja uso wakiwa tumboni.
Utafiti huo uliofanywa kwa kupiga
picha za Ultrasound, ulionyesha
kuwa vijusi hujifunza kusonga na
kuonyesha hisia wakati wakiwa
tumboni.
Picha hizo zilionyesha hisia za
vijusi hao wakati wa ujauzito
wakionekana wakicheka, au
kutabasamu, kukunja uso na hata
kuvuta pua.
Mtafiti mkuu Daktatri Nadja
Reissland, alisema kuelewa namna
ambavyo mtoto anakuwa tumboni,
inaweza kuwasaidia madaktari
kujua ikiwa kuna matatizo yoyote
na watoto kabla ya kuzaliwa.
"haijulikani ikiwa vijusi wanaweza
kuhisi uchungu au haijulikani ikiwa
kwa kukunja uso ni ishara tosha
kuonyesha ikiwa vijusi wanahisi
uchungu,'' alisema daktari huyo.
Utafiti ulionyesha kuwa mkunjo wa
uso ni dalili ya ubongo kukuwa
kuliko kuonyesha hisia za uchungu.
Utafiti ulitumia kanda ya video
iliyokuwa na picha tatu za
Ultrasound za vijusi wanane
wasichana na saba wavulana.
Utafiti huu unakuja baada ya
utafiti uliofanywa hapo awali
ukipendekeza kuwa vijusi wenye
afya nzuri huendelea kukuwa
wakati ujauzito ukiendelea
kukoma.
Daktari Reissland, mtafiti mkuu
katika chuo kikuu cha Durham,
amesema kuwa ni muhimu kwa
vijusi kuonyesha hisia za uchungu
mara wanapozaliwa ili waweze
kuonyesha ikiwa wana uchungu
huku wakirahisisha mawasiliano na
wazazi wao.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.