Breaking News
recent

Familia ya Mandela yakosoa wanahabari

Taarifa kutoka Ikulu ya Afrika
Kusini zinasema kuwa hali ya
kiafya ya rais mstaafu Nelson
Mandela sio nzuri na kuwa
imezorota katika saa 48
zilizopita.
Baada ya kumtembelea
hospitalini, mwanawe mkubwa
wa kike Makaziwa, alisema hali
inaonekana kuwa mbaya lakini
akaongeza kuwa Mandela
anaweza kuwasikia jamaa zake
wanapomuita huku akijaribu
kufungua macho yake. kiongozi
mashuhuri duniani, haimaanishi
utu wake udhalilishwe pamoja na
kuvuka mipaka kuingilia mambo
yake binafsi. Hapa naona kuna
ubaguzi wa rangi, huku vyombo
vingi vya kimataifa vikivuka
mipaka, ni kama ndege aina ya
Tai au Vulture wanaosubiri Simba
kumla mnyama aliomuwinda
kisha wakimbilie mzoga.
Wamevuka mipaka ya maadili.
Wakati hayati Margaret Thatcher
alipokuwa mgonjwa mbona
sikuona ukaribu wa vyombo vya
habari kiasi ninachokiona kwa
babaangu? Ni kwa sababu hii ni
nchi ya kiafrika. wanahisi kuwa
hapa wanaweza kuvuka mipaka
wanavyotaka, '' alisema
Makaziwe
Mapema leo, Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma alifutilia mbali
ziara yake ya kwenda Musumbiji
baada ya kumtembelea
hospitalini aliyekuwa Rais wa
Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais Zuma amesema kuwa
Bwana Mandela yuko katika hali
mbali ya afya.
Uamuzi wa Rais Zuma kufutilia
mbali ziara yake ambako
alitarajiwa kuhudhuria mkutano
wa kikanda kuhusu uekezaji
anaonyesha wazi kuwa hali ya
Mandela inaendelea kuzorota
zaidi kulingana na mwandishi wa
BBC mjini Johannesburg Mike
Wooldridge.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.