Breaking News
recent

Mapendekezo ya wagombea huru TZ


Tume ya Mabadiliko ya Katiba
nchini Tanzania, imependekeza
wawepo wagombea huru katika
ngazi za uchaguzi mbalimbali
nchini humo. Hayo ni miongoni
mwa mapendekezo yaliyotangazwa
jijini Dar es salaam na Mwenyeketi
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Jaji Joseph Warioba wakati wa
uzinduzi wa Rasimu ya Kwanza ya
Katiba Mpya.
Jaji Warioba amesema pia wapo
wananchi waliopendekeza
kwamba, wagombea huru
waruhusiwe kugombea nafasi zote
isipokuwa nafasi ya urais. Jaji
Warioba amesema tume ilipitia
maoni hayo na kupendekeza
kwamba, wagombea huru
waruhusiwe kugombea nafasi zote
kuanzia ngazi ya Mwenyekiti wa
Mtaa hadi nafasi ya Urais.
Kadhalika Jaji Warioba amesema,
Tume pia imependekeza kwamba,
mgombea yeyote wa urais ili
athibitike kuwa ni mshindi
atalazimika kupata zaidi ya asilimia
hamsini ya kura, na kwamba
endapo mgombea hatafanikiwa
kupata asilimia hamsini uchaguzi
utarudiwa kwa kuangalia
wagombea wawili waliopata kura
nyingi.
Mapendekezo mengine
yaliyotangazwa na Tume ni pamoja
na kuwepo kwa serikali tatu yaani
ya Bara,Zanzibar na ile ya
Shirikisho.
Pia tume imependekeza kuwa,
Bunge la Muungano liwe na jumla
ya Wabunge 75, hamsini kutoka
Bara, ishirini kutoka visiwani na
watano wateuliwe na Rais kutoka
makundi maalum ya walemavu.
Mapendekezo mengine ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ni pamoja na
Rais kubakia na madaraka yake ya
uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu,
lakini uteuzi wa ngazi za chini
uachiwe Tume ya Utumishi.
Imeeleza kwamba, Rais mara
baada ya kufanya uteuzi wa
viongozi wa ngazi za juu
wakiwemo, mawaziri, manaibu
waziri, jaji mkuu na naibu jaji
mkuu, viongozi hao watalazimika
kuthibitishwa na Bunge.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.