Breaking News
recent

Marekani yatoa onyo kwa raia wake Misri

Serikali ya Marekani imetoa
tahadhari kwa raia wake kutosafiri
nchini Misri huku ikiwataka
maafisa ambao hawajaajiriwa
katika ubalozi wake nchini humo
kuondoka mara moja kutokana na
ghasia zinazoendelea .
Baadhi ya raia wamefariki huku
wengine wengi wakijeruhiwa
vibaya kufuatia makabiliano kati ya
wafuasi wa rais Mohammed Morsi
na wale wa upinzani wakati
ambapo rais huyo anatarajiwa
kuadhimisha mwaka mmoja tangu
achukue hatamu.
Maafisa nchini Misri wanasema
kuwa kati ya waliouawa ni raia wa
marekani mjini Alexandria.
Tayari wananchi wa taifa hilo
wameanza kununua chakula na
mafuta kwa wingi ili kukihifadhi
kwa hofu kwamba ghasia hizo
huenda zikaenea.
Wapinzani wa rais Morsi wanadai
kuwa ameshindwa kutatua
maswala nyeti nchini humo huku
wafuasi wake wakisisitiza kuwa ni
sharti apewe mda.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.