Breaking News
recent

Mume na mke watoana jasho mahakamani

Mahakama ya rufaa nchini
Uingereza imebatilisha uamuzi
uliotolewa na mahakama kuu mjini
London, uamuzi ambao huenda
ukawa na athari kubwa kwa
wanandoa wanaokwenda
mahakamani kutalikiana.
Mahakama hiyo ya rufaa iliagiza
kuwa mali na hisa ya mfanya
biashara mmoja raia wa Uingereza
mwenye asili ya Nigeria, katika
kampuni mbali mbali zijumuishwe
katika orodha mali
watakayogawana.
Kufuatia uamuzi huo, agizo la
awali lililotolewa na mahakama
kuu ya hisa na mali anayomiliki
kupitia kampuni tofauti na watu
wengine isijumuishwe kama mali
ya mtu binafsi sasa imefutiliwa
mbali.
Majaji katika mahakama hiyo ya
rufaa waliagiza kuwa mali yote
inayomilikiwa na mfanyabiashara
huyo binafsi na katika makumpuni
tofauti katika sehemu mbali mbali
duniani ni lazima yajumuishwe.
Mkewe, tajiri huyo, Yasmin Prest
amesema amefurahishwa sana na
uamuzi huo wa mahakama.
Lakini Bwana Prest alifahamishwa
mahakama kuwa, hamiliki pekee
mali yake inayokisiwa kuwa
mamilioni ya madola.
Hata hivyo majaji hao walisema
kuwa uamuzi wa mahakama kuu
uliotolewa Oktoba mwaka uliopita,
wa kumlazimisha bwana Prest
kuhamishwa mali yake kutoka kwa
kampuni anazomiliki kwa pamoja
na watu wengine, sio halali.
Lakini Bi. Prest alikwasilisha rufaa
katika mahakama ya juu zaidi
kutoka kesi hiyo kusikilizwa upya.
Katika uamuzi wake mahakama
hiyo ya rufaa ilisema kuwa
kampuni hizo tofauti zinamiliki
mali hiyo kwa niaba ya bwana
Prest.
Kesi hiyo sasa itaangaziwa
pakubwa na familia tajiri, hasa
wale kutoka nje ya Uingereza.
Kwa mujibu wa wakili mmoja
William Longrigg, mahakama
imeonekana kuanza kuwalinda
wanyonge na wale wasiokuwa na
mali katika ndoa.
Vile vile amesema uamuzi huo wa
kubainisha kuwa mali
inayomilikiwa na kampuni ni mali
ya mtu binafsi ni mwanzo wa
kutambua mali hasa kwa wale
wanaoficha mali yao katika
makampuni wakati
wanapotengana na wakeo.
Mahakma hiyo ilifahamishwa kuwa
Prest ana mali inayokisiwa kuwa
pauni milioni 48, lakini mkeo
alikanusha madai hayo na kusema
kuwa huenda ni inazidi pauni
milioni mia moja.
Wawili hao walifunga ndoa mwaka
wa 1993 na tangu wakati huo
wamekuwa wakiishi mjini London.
Wakati wa kesi, Bwana Prest
alituhumiwa kwa kukosa kusema
ukweli kuhusu mali yote
anayomiliki.
Jaji Lord Sumption alisema kuwa
ushahidi wake ulijawa na
udanganyifu mkubwa na alijaribu
kuficha ukweli wa mambo.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.