Breaking News
recent

Marekani inadaiwa kufanya udukuzi duniani

Wizara ya sheria nchini Marekani
imeanzisha uchunguzi kwa kile
inachosema ni ufichuzi wa taarifa
za siri uliofanywa na mtaalamu wa
zamani wa mitambo wa Komputa
katika shirika la ujasusi wa
Marekani Edward Snowden.
Bwana Snowden alijitambulisha
baada ya kufichua kuwa mashirika
ya ujasusi nchini Marekani hufanya
udukuzi kote duniani kwa kutumia
mbinu ya kiteknolojia ya siri
kuchunguza mawasiliano ya simu
ya watu, barua pepe na
mawasiliano mengine.
Ufichuzi wa Edward Snowden
kuhusu shughuli hizo za kisiri
zinazojumuisha kudukua mitandao
yainternet na mawasiliano ya
simu, umezusha wasiwasi kote
ulimwenguni kuhusu kiwango cha
ukusanyaji wa taarifa hizo za
kijasusi Marekani.
Waziri wa mambo ya nje wa
Uingereza, William Hague,
anatarajiwa kutoa tamko rasmi
bungeni baadaye leo kuhusu
tuhuma kwamba mashirika ya
kijasusi Uingereza yalitumia data
iliyokusanywa namashirika ya
kijasusi Marekani kubadili sheria
kali nchini humo kuhusu taarifa za
siri.
Kwenye mahojiano na jarida la
Guardian,Edward Snowden ,
alisema kuwa wamarekani,
wanahujumu mamlaka ya serikali
na kutishia demokrasia.
Hatua ya Snowdon, imesababisha
wasiwasi kuhusu uwezo wa
Marekani kukusanya taarifa za
kijasusi ambao anasena ni
mkubwa mno.
Aliambia jarida hilo kuwa jambo
inalofanya Marekani ni la kutisha
akiongeza kuwa wao huvamia
mitandao na pindi mtu
anapowasha mtambo wake
wanaweza hata kuutambua
mtambo wenyewe na mtu
anayeutumia. Alisema kuwa mtu
hawezi kuwa salama licha ya ulinzi
unaotoa ili kuzuia uvamizi wa
mitandao.
Aidha alisema kuwa ''sitaki kuishi
katika jamii ambayo inafanya
mambo kama haya., sitaki kuishi
katika jamii ambayo kila
ninachokisema kinarekodiwa.''

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.