Muigizaji wa filamu nchini Jaji
Khamis (Kashi) amefariki dunia
mchana huu katika hospitali ya
taifa ya Muhimbili jijini Dar es
Salaam.
Kashi amewahi kutamba na
mchezo wa ITV, Tamu Chungu
akiwa na wasanii wenzake kama
Mzee Masinde,Samson na
wengine.
Baada ya kupata habari hii,
Mitandao mbalimbali imeongea na muigizaji
mwenzake Monalisa ambae
amethibitisha kutokea kwa
msiba huo. Monalisa amesema
alipata taarifa jana kwamba
Kashi amelazwa hospitali akiwa
amezidiwa kiasi cha kushindwa
kuongea na hivyo kushindwa
kujua nini kilikuwa
kinamsumbua.
Naye Hemedy PHD ametweet:
REST IN PEACE MUIGIZAJI
MWENZETU JAJI KHAMIS
KASHI….MUNGU AKULAZE
PEMA PEPONI…MOVIE YA
MWISHO TULICHEZA WOTE
ILIKUA MATILDA!!Sad newz
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment