Breaking News
recent

Hatimaye Reginald Mengi awakabidhi zawadi washindi wa ‘tweet’ zilizomgusa kwa mwezi.

May 13 mwaka huu mwenyekiti
wa makampuni ya IPP bwana
Reginald Mengi alitangaza ulaji
ambao ni kama wa bure, kwa
kutangaza shindano la ‘tweet’,
ambapo alisema kila mwezi
atakuwa akitoa zawadi ya
shilling million 1 kwa mtu
atakaye andika tweet bora
kushinda vita dhidi ya
umasikini.
Inawezekana wapo ambao
walihisi kuwa huenda bwana
Mengi alikuwa anatania, lakini
amethibitisha ni kiasi gani
hakua anatania baada ya jana
(June 7) kuwakabidhi washindi
watatu zawadi zao za pesa.
Bwana Mengi alimkabidhi
mshindi wa kwanza Jilly
Gaudence Kyomo zawadi yake
ya shillingi millioni 1,
aliyefuatiwa na mshindi wa pili
ni Peter George aliyejishindia
shillingi 500,000 na mshindi wa
tatu Ludovick Angelino
aliyejipatia shillingi 400,000.
Washindi hao walikabidhiwa
zawadi zao katika hafla fupi
iliyofanyika katika ofisi za
makao makuu ya IPP jijini Dar
es salaam, na baadae bwana
Mengi alitweet kuwapongeza
washindi.
Kwa mujibu wa chanzo, bwana
Mengi alisema shughuli ya
kupata washindi hao ambao
walichujwa kutoka katika tweet
481 zilizokuwa zilizopokelewa
toka (Mei 13) siku alipozindua
shindano hilo, ilisimamiwa na
Kiongozi wa Taasisi ya Chuo
cha Uongozi na Ujasiliamali
(IMED), Donath Olomi na jopo
lake.
Tweet iliyompa Jilly ushindi wa
nafasi ya kwanza ilikuwa ‘Tuwe
na utamaduni wa kupenda kile
tukifanyacho, tukifanya kwa
moyo, uadilif, heshima na kujali
muda hata kama it’s self
employed”, ambayo ilitimiza
vigezo vya shindano ambavyo
vilikuwa liwe wazo lililoeleweka
na kuelezeka kirahisi, na lisiwe
limeshasikika mara nyingi.
Haya kazi kwenu jamani
shindano bado linaendelea kila
mwezi kwa muda wa mwaka
mzima so kuna miezi 11 mbele
ya ulaji huo, washindi
watakuwa wanakabidhiwa
zawadi zao na kutangazwa.
Picha ni kutoka akaunti ya
twitter ya Reginald Mengi

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.