Rapper wa Mwanza, Kala
Jeremiah amefanikiwa kuibuka
na tuzo tatu ikiwemo kubwa ya
wimbo bora wa mwaka kwa hit
yake ‘Dear God’. Kala alishinda
pia tuzo ya msanii bora wa Hip
Hop kwa kuwabwaga Fid Q, Joh
Makini, Profesa Jay na Stamina
kwenye kipengele hicho.
Naye Ommy Dimpoz ameibuka
na tuzo tatu zikiwemo za wimbo
bora wa Bongo Pop na wimbo
bora wa kushirikiana/
Kushirikishwa kwa hit single
yake Me and You. Pia hit yake
Baadaye imechukua tuzo ya
video bora ya mwaka.
Licha ya kutokuwepo wala
kutuma mwakilishi, Diamond
alifanikiwa kushinda tuzo kubwa
ya pili kwa usiku huo ya msanii
bora wa kiume kwa kuwabwaga
Ben Pol, Linex, Mzee Yusuf na
Ommy Dimpoz na pia kushinda
tuzo ya Msanii bora wa kiume
Bongo Flava.
Tuzo za muziki wa dance
zilitawaliwa na Chalz Baba wa
Mashujaa Band aliyeibuka tuzo
mbili za Msanii bora wa kiume
Bendi na Mtunzi bora wa
mashairi – Bendi.
Usiku wa tuzo za KTMA
ulipambwa na burudani ya aina
yake kutoka kwa wasanii
mbalimbali wakiwemo Linah,
Amini, Richie Mavoko,
Mataluma, Hussein Jumbe,
Zahir Zorro, Patricia Hillary na
Barnaba. Wengine ni Snura,
Godzilla, Mabeste, Madee na
Afande Sele.
Host wa tuzo hizo mwaka huu
alikuwa ni ZEMBWELA na TJ.
Uncategories
Kala Jeremiah, Ommy
Dimpoz, Diamond na
Chalz Baba waibuka na
tuzo nyingi zaidi kwenye
KTMA 2013
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Yep yep! Bongo tunaingia kwny chati thc time around.....
ReplyDelete