Umoja wa mataifa unasema kuwa
kiongozi mmoja mkuu wa kundi la
wapiganaji wa kiisilamu nchini
Somalia, al-Shabab, Hassan Dahir
Aweyes, amejisalimisha kwa
wanajeshi wa Somalia.
Bwana Aweyes alitafuta hifadhi
mjini Adado,mji ulio umbali wa
kilomita miatano kaskazini mwa
Mogadishu baada ya mapigano
makali kati ya mirengo ya Al
Shabaab mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa kiukoo, wamekwenda
huko kujadili watakachofanya naye
baada ya kujisalimisha kwake.
Lakini viongozi hao
wamefahamisha mwandishi wa
kituo cha utangazaji cha uingereza
BBC kuwa amekanusha madai
kuwa amejisalimisha na kwamba
amekataa kusafiri kwenda
Mogadishu.
Bwana Aweyes amekuwa
akijulikana kama kiongozi mkubwa
katika kundi la al-Shabab na Umoja
wa mataifa na Marekani
zinamfahamu kama gaidi
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment