Leo hii nimepita ukurasa
wamsanii bora wa hiphop,
mtunzi bora na aliechukua tuzo
ya wimbo bora wa mwaka, Kala
Jeremiah, na kukutana na
ujumbe aliouandika akitangaza
kutoa tuzo moja kwa marehem
Albert Mangweha a.k.a Ngwea
na kuikabidhi kwa mama mzazi
wa marehem Albert Mangwea.
''tAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI NA UMMA KWA UJUMLA.
mIMI KAMA MSANII BORA WA
HIP HOP KWA MWAKA HUU
NAPENDA KUCHUKUA MUDA HUU
KUWATANGAZIA WATU WOOTE
KUWA. KATIKA TUZO TATU
NILIZOCHUKUA MOJA
NAIKABIDHI KWA ALBERT
MANGWEA.YANI NI TUZO YA
MANGWEA NA NITAIPELEKA KWA
MAMA MZAZI WA MANGWEA
MOROGORO.
NIMEAMUA HAYO KWA KUWA
HAYATI ALBERT MANGWEA
ALIKUWA ANAFANYA MZIKI
AMBAO UKO UPANDE AMBAO
MIMI NIMESHINDA TUZO TATU
YANI HIP HOP.
TUZO NILIYOAMUA KUMPA
MANGWEA NI TUZO YA MSANII
BORA WA HIP HOP. KWA KUWA
ALIKUWA ANASTAHILI PIA
KUITWA HIVYO
TUZO HII NAAMINI ITAKUWA
UKUMBUSHO MHIMU SANA KWA
FAMILIA YAKE.LAKINI PIA
ITAKUWA INAONYESHA
MSHIKAMANO WETU KAMA
WASANII WA HIP HOP.''
POPOTE ULIPO KAMA WEWE NI
SHABIKI WA HIP HOP TAFUTA
NJIA YOYOTE YA KUENDELEA
KUMUENZI NDUGU YETU
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI HIP HOP.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment