Hivi karibuni Diamond aliamua
kuweka ‘ego’ pembeni na kukiri
kuwa Jokate Mwegelo ndiye
msichana katika maisha yake
aliyemkosea sana na anajuta
kumuumiza.
Diamond alifunguka hayo
kwenye kipindi cha Take One
cha Clouds TV, kilichorushwa
wiki iliyopita.
Akiongelea jinsi alivyomuumiza
Jokate, Diamond alisema,
“Kwasababu alikuwa too
innocent halafu hakuwahi
kunikosea kitu chochote Jokate
kabisa, halafu nikamwingiza
kwenye matatizo, watu
wakamchukulia tofauti kwamba
‘Jokate kamchukulia Wema
boyfriend wake’ wakati
nilimfuata mimi kama mimi,
nilimtafuta mwenyewe halafu
then nikawa niko naye halafu
ghafla nikarudisha mahusiano
kwa Wema. Sikujiskia vizuri
halafu still haikuwa vizuri so
sometimes nikikaaga hivi
nasema nilimkosea.”
Akijibu swali la kwanini
alimuacha Jokate, Diamond
aliongeza, “Sijui nilirogwa hata
sijui, I don’t know, sijui hata
kwanini, hakuwahi kunikosea
chochote sio, sababu nilikuwa
nikikaa naye alikuwa akinishauri
vitu vingi vya maendeleo, sijui
ulikuwa ni utoto sielewi yaani,
sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya
sana, halafu mtoto wa watu
mstaarabu sana, alijitahidi
kujenga career yake sasa hivi
imekaa vizuri.”
Bongo5 imewasiliana na Jokate
ili kutaka kufahamu upande
wake baada ya kusikia kauli ya
Diamond aliyesema anafurahi
kuona Diamond amefunguka
ukweli.
“Watu wengi hawajui the real
issue, I’m glad kama ame-
acknowledge I was innocent in
that whole matter,” amesema
Jokate.
Uncategories
Exclusive: Jokate aongea
baada ya Diamond kukiri
kuwa anajuta kumkosea
na kuuvunja moyo wake
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment