Breaking News
recent

Wabunge Uingereza wamjadili Trump.

Wabunge wa Uingereza wamekuwa na mjadala kuhusu kupigwa marufuku au la kwa anayewania nafasi ya kupeperusha bendera ya chama cha republican katika kinyang'anyiro cha urais wa Marekani, Donald Trump kuingia nchini Uingereza.
Mjadala huo uliochukua muda wa saa tatu umekuja baada ya karibu nusu milioni ya watu nchini Uingereza kuunga mkono hatua ya kumzuia Trump kuingia Uingereza. baada ya Trump kusema kuwa Waislamu wote wazuiwe kuingia marekani ikiwa ni njia ya kupambana na vitendo vya kigaidi
Wabunge hata hivyo hawakuonyesha shauku kubwa ya kumfungia milango Trump ili asiingie Uingereza kwani hakuna kura yeyote iliyopigwa mwishoni mwa mjadala
Mmoja wa wabunge wa Uingereza ambaye ni muislamu amesema kauli za Trump ni sumu, huku msemaji wa idara ya mambo ya ndani Jack Dromey akisema kuwa Trump azuiwe kuingia Uingereza.
Wakati huo huo Trump ameendelea na kampeni zake, akizungumza katika chuo cha Liberty, chuo binafsi cha kikristo kilicho Lynchburg, Virginia amewaambia wanafunzi wa kikristo kuwa wanapaswa kuungana kuilinda dini yao.
''Tunapaswa kuilinda kwa kuwa kuna mambo yanafanyika, mambo mabaya sana, sijui ni nini lakini hatuungani labda.dini nyingine wanaungana kuzuia, hapa tunayo...ukitazama nchi hii, asilimia 70 mpaka 75 ni wakristo, watu wengine wanasema hata zaidi ya hiyo, inadhihirisha nguvu tuliyonayo, tunapaswa kuungana'' alieleza Trump katika kampeni yake.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.