Breaking News
recent

Sipendi kufananishwa na rappers wengine – Joh Makini.....

Joh Makini anaamini kumfananisha na rappers wengine ni kutengeneza chuki.
Akiongea na XXL ya Clouds Fm, Joh Makini amesema hapendi kabisa kufananishwa na rapper wengine kwasabu hivyo vitu havijengi, vinabomoa
“Sipendi kwasababu mimi tangu naanza mziki wangu nacheza kwenye level zangu… kama unanifatilia utagundua nna njia yangu kabisa napita mwenyewe, sio kitu kibaya watu kukufananisha kwasababu wote tunafanya hiphop na vitu kama hivyo, wakati mwingine unajua hivi vitu vinazua hata chuki nawatu kutengeneza picha ambazo ni tofauti , na wewe unaweza kuwa shaidi sisi kama weusi hujawahi kutusikia tukimuongelea msanii yoyote tofauti au kutengeneza, tunajaribu sana kukwepa hivyo vitu  kwasababu tushagundua havijengi Industry vinabomoa, Kwahiyo sisi tunalenga sana kwenye kujenga na lengo letu kubwa ni kuendelea kuibrand hiphop ya Tanzania kwenda kwenye level nyingine kibiashara” Joh Makini alielezea.
Joh Makini anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Don’t bother aliomshirikisha rapper Aka.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.