Breaking News
recent

Don Jazzy na Olamide wapatana baada ya kurushiana maneno makali kwenye Tuzo za The Headies....

Wasanii wa Nigeria, Don Jazzy na Olamide wamepatana baada kurushiana maneno makali kwenye Tuzo za The Headies 2015 zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Don Jazzy na Olamide wote wameweka picha moja na ujumbe mmoja kwenye mitandao ya kijamii kuwaonesha mashabiki wao kuwa wamemaliza tofauti zao, wameandika
“We are very sorry for the wahala. Make una no vex ooo. It is our responsibility to lead but then again we re only human and we all make mistakes. #WeAreSorryHeadies #WeAreSorryFans #PeaceAndUnity #YBNL #SMD #OneLagos #OneNigeria”
Ugomvi wa wasanii hao nguli wa Naija ulianza siku ya Utoaji wa Tuzo za The Headies baada  Reekado Banks, aliye chini ya Mavin Records ya Don Jazzy kumshinda msanii aliye kwenye lebo moja na Olamide, Lil Kesh na kushinda tuzo ya ‘The Next Rated Award.’ ambayo ilikua inakuja pamoja na zawadi ya gari aina ya  Hyundai suv.
Olamide Alipopanda jukwaani akiwa na crew nzima YBNL aliamua kufunguka ya moyoni  baada ya msanii wake Adekunle Gold kushinda tuzo ya Best Alternative akipondea ushindi wa Reekado Banks akidai kuwa Tuzo hiyo alistahili kupata Lil Kesh
“This award belongs to Lil Kesh. Lil Kesh is our own Next Rated artist. F**k that shit! The streets ti take over. Every f**king single was a hit back to back. From lyrically to Shoki to Efejoku. Ko ni dafun Iya anybody”, alisema Olamide, kutupa mic chini na kuondoka.
Don Jazzy aliyeshinda tuzo ya “Lifetime Achievement Award” alimjibu Olamide kwa kumuambia kama anataka gari la ushindi wa tuzo aliyoilalamika anaruhusiwa kwenda kuichukua.
“Egbon Olamide, if you want the car, come and take it,” alisema, Tazama Video ya Drama nzima hapo chini
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.