Breaking News
recent

Rais Obama amwaga machozi wakati akitoa hotuba kuhusiana na mipango ya kudhibiti Silaha

Huku machozi yakitililika mashavuni kwake, Rais wa Marekani Barack Obama alitoa hotuba kuhusiana na mipango ya kudhibiti Silaha huko Washington, DC.
Katika hotuba yake iliyojaa kila aina ya hisia kali, Rais Obama amebainisha wazi mipango yake juu ya kuweka mikakati thabiti ya udhibiti silaha za moto, akisema kwamba Marekani haipaswi kukubali mauaji kama gharama yoyote.
Obama amesema kwamba hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa ambazo zitajumuisha ufuatiliaji wa tangu awali wa upatikanaji silaha, pia uchunguzi wa afya ya akili utazingatiwa na hii ni pamoja na kumbukumbu za uhalifu wa mtuhumiwa zitahusishwa pia.
Rais Obama anatarajiwa kuweka hadharani hatua zitakazochukuliwa dhidi ya matumizi mabaya ya silaha na hasa ikizingatiwa hii ni miaka ya upinzani mkali katika serikali yake.
Hata hivyo chama cha wauza silaha nchini Marekani kimekosoa hotuba ya Rais na kusema kwamba mapendekezo yake hayatazuia mauaji ya halaiki kutokana na aliyoyasema katika hotuba yake.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.