Breaking News
recent

MWANAUME WA KWANZA DUNIANI KUBEBA MIMBA AJIFUNGUA MTOTO WAKE SALAMA

Yule mwanamke-mwanaume
wa Marekani ambaye alijipatia
umaarufu mkubwa mwaka
jana baada ya picha yake
akiwa na mimba huku akiwa
na midevu kusambaa duniani
amerudi tena kwenye vichwa
vya habari mwaka huu baada
ya kujifungua mtoto wa pili.
Thomas Beatie, au maarufu
kama 'Mwanaume Mjamzito'
amerudi tena kwenye vichwa
vya habari vya magazeti baada
kujifungua kwa mara ya pili
mtoto wa kiume jana asubuhi.
Picha za Thomas akiwa na
madevu kibao huku akiwa na
tumbo kubwa la ujauzito
zilikuwa maarufu sana duniani
mwaka jana kiasi cha
kumfanya Thomas atajwe
kama mwanaume wa kwanza
kupata ujauzito.
Thomas anaishi na mkewe
Nancy ambaye ndiye
atakayekuwa akimnyonyesha
mtoto wao mpya kama
alivyofanya kwa mtoto wao wa
kwanza wa kike anayeitwa
Susan Juliette aliyezaliwa
mwezi juni mwaka jana.
Thomas alizaliwa kama
mwanamke lakini baadae
alibadilisha jinsia kuwa
mwanaume na kufanya
upasuaji wa kuondoa matiti
yake huku akitumia madawa
ya homone za kiume
yaliyomfanya awe na madevu
kama mwanaume.
Thomas hakufanya upasuaji
wa kuondoa uke wake hali
ambayo ilimwezesha kupata
ujauzito wa mtoto wake wa
kwanza baada ya
kupandikizwa mbegu za
kiume.
Thomas ambaye hivi sasa ana
umri wa miaka 35 alisema
kuwa aliamua kuzaa mtoto
baada ya mke wake Nancy
mwenye umri wa miaka 45
kutokuwa na uwezo wa
kushika ujauzito.
"Kuwa na mtoto hakuangalii
kuwa wewe ni mwanamke au
mwanamme, mimi pia ni
binadamu na ninahitaji kuwa
na mtoto " alisema Thomas.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.