Breaking News
recent

MWANAUME ALIYEKUWA AKIJIFANYA NI " JOKATE MWEGELO" HUKO FACEBOOK AKAMATWA NA POLISI

Hapa ni wakati Jokate
alipoamua kukaa na Mpeka
kistaarabu kuongea nae kabla
ya hatua za kisheria
Message alizotumia watu
kwenye facebook na msg za
simu za mkononi.
Aliyefanikisha huyu jamaa
kukamatwa ni mrembo mmoja
model Blessing ambae
alishiriki Miss Morogoro 2013
ambapo namkariri akisema:
“W iki mbili zilizopita nilipata
msg kwamba Kidoti hair na
Mzinga Planet wanahitaji
mamodo kwa ajili ya
kutengeneza matangazo kwa
ajili ya nywele za kidoti,
tulikua Morogoro kwa ajili ya
Miss Morogoro tukaja Dar
mpaka Mzalendo Pub msg
ilipotuelekeza lakini
nilivyoingia sikuona mtu
ambae anahusiana na Jokate,
niliona watu ambao nawajua
lakini sio kuhusu nywele .
"Nikampigia kaka mmoja
anaitwa Johnson kwa sababu
najua anafahamiana na Jokate,
nikampigia kumfokea
kumwambia nyinyi vipi mbona
mmetangaza audition alafu
sioni hata mtu mmoja ambae
anahusika? naona watu ambao
kampuni zao zipo majumbani
kwao?
"Baada ya dakika zaidi ya 10
kina Jokate wakawa
wameshafika japo baadhi ya
mamodo wengine walikua
wameshaondoka lakini baadhi
ya viongozi kama Majaji wa
kike walikuwepo na
walipoulizwa wakasema
tumsubiri Mpeka ambae ndio
muhusika na pia Mkurugenzi
wa Mzinga Planet” – Blessing
Baada ya kina Jokate kufika
Mpeka alipigiwa simu ili arudi
Mzalendo Pub, japo alisita sana
mtuhumiwa huyu alikuja
kwenye eneo la tukio na
kukutana uso kwa uso na
Jokate na timu yake, baada ya
hapo akaanza kusingizia
kwamba yeye hahuusiki ila
kuna watu wengine ndio
wanahusika ila alipotoa namba
zao wakapigiwa simu, kila
mmoja alionekana kutaharuki
kwa sababu hawajui chochote
kuhusu hiyo Mzinga Planet.
Baada ya Jokate na timu yake
kukaa na Mpeka na kumuuliza
kistaarabu bila kutoa
ushirikiano wa kutosha,
uamuzi ulitoka kwamba
apelekwe Polisi Osterbay ili
kuendelea na taratibu nyingine
za kisheria.
Mpeka alikua anaonekana
analia wakati mwingine na hiyo
ilikua ni baada ya kumpiga
huyu msichana shuhuda
aitwae Blessing kwa sababu
alimchomea mpaka
akakamtwa.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.