Breaking News
recent

Hali ya Mandela imeimarika asema Bi. Machel

Mke wa Nelson Mandela, Graca
Machel amesema kwa sasa hana
wasi wasi sana kuhusu afya ya rais
huyo wa zamani wa Afrika Kusini
kama ilivyokuwa wiki chache
zilizopita.
Bi Machel amesema hali ya
Mandela inaendelea kuimarika kila
uchao.
Mandela ambaye ni rais wa
kwanza mweusi wa Afrika Kusini,
mwenye umri wa miaka tisini na
nne, anasemekana kuwa katika
hali mahututi.
Mandela alilazwa hospitalini wiki
tano zilizopita na hapo jana rais
wa Afrika Kusini, Jacob Zuma,
alisema kuwa mwanaharakati huyo
wa uhuru amesalia kuwa
mpiganiaji mkubwa kama
alivyokuwa miaka hasmini
iliyopita.
Mandela alilazwa hospitalini
tarehe nane mwezi Juni, kutokana
na maambukizi ya mapafu.
Wiki iliyopita, rais Zuma alipuuzilia
mbali madai kuwa afya ya Bwana
Mandela imezorota kiasi kwamba
hawezi kupona tena.
Watu kadhaa ambao
wamemtembela hospitalini
wamesema kuwa Bwana Mandela
angali ana ufahamu na anaweza
kujibu na kuitikia salamu.
Mwandishi wa BBC Mjini
Johannesburg, amesema kuwa Bi.
Machel amekuwa kando ya
mumewe tangu alipolazwa
hospitalini na amejiepusha na
mzozo unaokumba familia ya
Bwana Mandela kwa wiki kadhaa
zilizopita.
Maafisa wa serikali ya Afrika Kusini
wametoa wito kwa raia wa nchi
hiyo kujiandaa kwa sherehe za
kuadhimisha miaka tisini na tano
ya kuzaliwa kwa Bwana Mandela
wiki ijayo.
Mandela anaenziwa kote duniani
kutokana na juhudi zake za
kumaliza utawala wa ubaguzi wa
rangi nchini Afrika Kusini.
Alifungwa miaka 27 gerezani kabla
ya kuachiliwa huru mwaka wa
1990 na kuchaguliwa kuwa rais wa
kwanza mweusi wa Afrika Kusini
mwaka wa 1994.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.