Breaking News
recent

HIZI NI SABABU NA MATIBABU ZA HARUFU MBAYA SEHEMU ZA SIRI (VAGINOSIS) ZA MWANAMKE

Kitaalamu hali ya mwanamke
kutokwa na majimaji yenye
rangi nyeupe au ya njano, ni
hali ya kawaida na wala siyo
tatizo endapo majimaji hayo
siyo mazito sana na wala
hayatoi harufu mbaya.
Ila majimaji yanayotoka
yakiwa katika hali ya ute
mzito wenye rangi nyeupe au
kahawia na yakiwa yanatoa
harufu mbaya na yanawasha,
basi hiyo ni ishara ya ugonjwa
uitwao Vaginosis.
Majimaji au ute unaoteleza
kutoka sehemu za siri ni njia
inayowezesha viungo vya uzazi
vya mwanamke kujisafisha na
kuutoa uchafu wa seli
zilizokufa na mabaki ya damu
ya hedhi nje ya mwili.
Utokaji huo wa uchafu ni njia
ya kuvikinga viungo vya uzazi
dhidi ya maambukizi ya
bakteria au fangasi wanaoleta
magonjwa. Kwa kawaida huwa
hayatoi harufu na huwa na
rangi nyeupe au ya njano.
Pia huwa na asidi ya lactic
ambayo huzuia kuzaliana kwa
vijidudu vya maradhi na
huzalishwa kwenye tezi za
Bartholin. Kwa kawaida,
mwanamke hutoa kiasi cha
gramu 2 za seli zilizokufa
kutoka kwenye mji wa uzazi na
gramu 3 za ute mwepesi kila
siku.
Kiwango hiki huweza
kuongezeka au kupungua
kutegemeana na mzunguko wa
hedhi. Kuna wakati ute huwa
mwepesi na unaovutika (kama
ute wa yai la kuku) na kuna
wakati huwa mzito kiasi na
wenye rangi ya njano.
Ute huu ni wa kawaida na
huwatoka wasichana au
wanawake wote baada ya
kuvunja ungo.
SABABU ZA KUTOA UTE
Katika uchunguzi wa
kitaalamu imegundulika kuwa
kuna mambo mengi
yanayosababisha mwanamke
kutoa ute au majimaji yasiyo
ya kawaida kwenye sehemu
zake za siri.
Maambukizi ya bakteria
wanaosababisha magonjwa
kama Trichomoniasis,
Candidiasis, Kisonono au
Gonorhear au uambukizo wa
bakteria Candida albicans na
Vaginosis husababisha
mwanamke kutokwa na uchafu
unaoambatana na harufu
mbaya.
Pia kukaa na pedi muda mrefu
sana bila ya kubadilishwa
wakati wa hedhi, huweza
kusababisha tatizo hili na
kuwa mazalia mazuri ya
bakteria wanaosababisha
harufu mbaya.
DALILI
Wanawake wenye tatizo la
Vaginosis huwa na dalili
kubwa ya kutokwa na
uchafu usiyo wa kawaida
sehemu za siri. Uchafu huu
huwa unatoa harufu kali kama
shombo ya samaki au kitu
kilichooza na huambatana na
maumivu makali ya tumbo
chini ya kitovu.
Tukasema kitaalamu hali ya
mwanamke kutokwa na
majimaji yenye rangi nyeupe
au ya njano, ni hali ya kawaida
na wala siyo tatizo endapo
majimaji hayo siyo mazito
sana na wala hayatoi harufu
mbaya.
Ila majimaji yanayotoka
yakiwa katika hali ya ute
mzito wenye rangi nyeupe au
kahawia na yakiwa yanatoa
harufu mbaya na yanawasha,
basi hiyo ni ishara ya ugonjwa
uitwao Vaginosis.
Tulieleza mengi na tukataja na
sababu za kitaalamu kuwa
imegundulika kwamba kuna
sababu nyingi ambazo
husababisha mwanamke kutoa
ute au majimaji yasiyo ya
kawaida kwenye sehemu zake
za siri.
Leo tutaeleza dalili kisha
tutaeleza vipimo na tiba ya
maradhi haya ya kike katika
jamii yetu.
DALILI
Wanawake wenye tatizo la
Vaginosis huwa na dalili
kubwa ya kutokwa na
uchafu usiyo wa kawaida
kutoka sehemu za siri. Uchafu
huu huwa unatoa harufu kali
kama shombo ya samaki au
kitu kilichooza na huambatana
na maumivu makali ya tumbo
chini ya kitovu.
Wakati mwingine uchafu
wenye rangi kama ya kijani
hutoka,kuwashwa sana
sehemu za siri, mgonjwa
asipopatiwa tiba haraka
husababisha vidonda sehemu
za siri kwa sababu ya kujikuna
kutokana na mwasho
anaoupata.
Kuna wakati mwingine
mwanamke anatokwa na ute
uliochanganyikana na damu
hata kama hayupo kwenye
siku zake, hii ni dalili nyingine
ya Vaginosis. Mgonjwa pia
anaweza kusikia maumivu
makali wakati wa tendo la
ndoa, hali ambayo pia inaweza
kusababishwa na kuingiwa
kwa bakteria katika mji wa
uzazi.
Bakteria hao huweza
kusababisha siyo harufu tu,
bali mgonjwa anaweza
kutokwa na usaha sehemu
hiyo ya siri.
MATIBABU
Tatizo hili hutibika hospitalini
baada ya vipimo vya
kitaalamu kuchukuliwa na
mtaalamu mwenye uzoefu wa
kutosha juu ya magonjwa ya
wanawake. Daktari anaweza
kumpa mgonjwa dawa za
kupaka na dawa za kumeza
ambazo huweza kumaliza
tatizo hili.
USHAURI
Mara nyingi nashauri kuwa ni
makosa kutumia dawa bila
kupata ushauri wa kitaalamu
kutoka kwa daktari aliye na
ujuzi wa magonjwa hayo na
siyo kupewa dawa na wauzaji
wa maduka ya dawa.
Nasema hivyo kwa sababu
watu wengi wana kawaida
kwenda kwenye duka la dawa
na kupewa dawa na muuzaji
bila kupimwa. Kumbuka
unaweza kupewa dawa
ambayo siyo ya ugonjwa wako.
Nawashauri pia wale
wanawake wenye kawaida ya
kutumia pafyumu au kuweka
dawa sehemu za siri kwa lengo
la kuzifanya kuwa ndogo,
waache kufanya hivyo kwani
madhara yake ni makubwa
sana kiafya likiwemo hilo la
kutoa harufu mbaya sehemu
hizo na zinaweza kusababisha
madhara makubwa katika njia
ya uzazi.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.