Breaking News
recent

HUYU NDIYE MTANZANIA ALIYEUWAWA NA VIBAKA JUZI ALHAMISI NCHINI MAREKANI....

POLISI wametambua mwili wa
mwanafunzi wa Howard
University aliyeuawa kwenye
jaribio la uhalifu Alhamisi usiku.
Omar Sykes, 22, na mwanafunzi
mwenzake walikuwa wanatembea
maeneo ya 700 block of Fairmont
Street NW kabla ya saa 5.30
usiku walipofuatwa na watu
wawili.
Polisi wanaamini kulikuwa na
jaribio la uhalifu ila yalitokea
mabishano kabla mmoja ya wale
watu kutoa bastola na kumuua
Sykes. Alifikia mauti kwenye
hospitali ya maeneo ya jirani.
“Tunadhani ilikuwa jambo la
ghafla na hatuna uhakika
kama wanafunzi hao waliibiwa
mali yoyote” alisema Kapteni
Bob Alder wa kituo cha polisi DC
alipohojiwa na News4.
Mwanafunzi mwingine alipigwa
na kitako cha bastola na
kujeruhiwa kichwani ingawa hana
majeraha makubwa.
“Wanafunzi wengi wamepatwa na
hofu ya kutoka na kutembea
usiku kwani hali hii inaogopesha
sana,” alisema mwanafunzi
mmoja alipohojiwa na Megan
McGrath kutoka News4.
Maelezo kamili kuhusu
watuhumiwa bado
hayajapatikana. Kulikuwa na
matukio mengi ya kujumuisha
watu wakati wa tukio hivyo polisi
wanatumaini kuwa haitawia
vigumu kwa wahalifu hao
kujulikana.
Sykes alipenda uandishi na mara
ya mwisho aliandika makala
kwenye mtandao unaoitwa Our
Black Pages mnamo tarehe 11
Juni. Wasifa wake unaonesha
kwamba alikuwa anasomea
Marketing na Public Relations.
Mkesha wa sala kwa ajili ya
marehemu utafanyika shuleni
kwao Jumamosi kuanzia saa 1
usiku.
Howard University imetoa
maelezo yafuatayo kuhusiana na
kifo cha Alhamisi:
“Tuna huzuni kubwa kufuatia
kifo cha mmoja wa wanafunzi
wetu kilichotokea nje ya shule.
Mwanafunzi mwingine
alijeruhiwa kwenye tukio hilo
na anaendelea na matibabu….
Polisi wa Howard University
wanashirikiana polisi wa mji ili
kupeleleza tukio hili hatari.
Tunawapa pole familia, shule
na wale wote walioguswa na
tukio hili kwa namna moja au
nyingine. Huduma ya ushauri
nasaha itapatikana masaa 24
kwa wa nafunzi wote
watakaohitaji msaada katika
kipindi hiki kigumu.”

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.