Breaking News
recent

Mchawi mtanzania jela miaka 3 Kenya

Vifaa walivyopatikana navyo
washukiwa walipokamatwa na
polisi
Mchawi kutoka Tanzania
amehukumiwa kifungo cha
miaka mitatu nchini Kenya kwa
kumlaghai mwanamke
mfanyabiashara mkenya na
kumuibia shilingi milioni tisa.
Mchawi huyo alimhadaa mama
huyo kuwa kwa kupitia njia za
kichawi angeweza kuzifanya pesa
hizo kuwa maradufu yaani milioni
18.
Bwana Amos Chipeta pia
ataongezwa kifungo cha miezi
tatu kwa kupatikana na vifaa
vinavyoumiwa kufanya uchawi
kama vile chupa, visu na ngozi ya
Paka.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily
Nation, Chipeta alihukumiwa
pamoja na mwenzake bwana
Peter Christopher aliyepatikana na
hirizi zinazotumika kufanyia
uchawi.
Bwana Chipeta alimlaghai Bi
Catherine Njeri hela zake tarehe
tofauti tofauti kati ya mwezi wa
Agosti na Decemba 2012 baada ya
mwanamke huyo kuwaendea na
kumwomba wazifanye pesa hizo
ziwe maradufu
Walijitetea kwa kusema kuwa
mwanamke huyo aliwaendea ili
wampe nguvu za kichawi aweze
kuwashinda wapinzani wake wa
kisiasa
Maafisa wa polisi walipata hirizi
hizo na vifaa walivyotumia kwa
uchawi mwezi Februari 1, 2014
katika nyumba ya kukodisha iliyo
kando ya barabara ya Juja
viungani mwa mji mkuu Nairobi.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo
alisema kuwa wanaume hao
waliona mwanamke huyo kuwa
mjinga na basi kumnafiki kwa
urahisi na kuwa hawana majuto
au toba.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.