Breaking News
recent

Apple kuinunua Beats kwa dola bilioni 3

Kampuni kubwa ya teknolojia
Apple imethibitisha kwamba
itanunua vipokea sauti na
huduma ya kusikiliza muziki
kupitia kwenye mtandao wa
inteneti kutoka kampuni ya
Beats Electronics katika
makubaliano ya dola bilioni 3.
Hayo yakiwa ni makubaliano
makubwa katika historia ya miaka
38 ya kampuni hiyo.
Hatua hiyo inaonekana kama
jitihada ya kuiendeleza sifa ya
Apple katika soko la kusikiliza
muziki kwenye mtandao.
Pamoja na ununuzi huo,
waanzilishi wa Beats Jimmy
Lovine na msanii mtajika katika
mtindo wa kufoka na Hip Hop Dkt.
Dre watajiunga na kampuni hiyo
ya kiteknolojia.
Apple kuinunua Beats kwa dola
bilioni 3
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya
Apple Tim Cook alisema kuwa
mkataba huo ungewezesha
kampuni hiyo ‘kuendelea
kutengeneza bidhaa na huduma
za muziki zenye ubunifu duniani.’
Beats ilianzishwa na mzalishaji wa
muziki Jimmy Lovine na nyota wa
mziki wa kufokafoka, Dr. Dre, na
mitambo hiyo imejulikana kuwa
bora zaidi hadi siku za hivi majuzi.
Beats ilianzisha huduma ya muziki
unaolipiwa mapema mwaka huu.
Apple ina huduma ya iTunes
ambayo ndio kubwa zaidi duniani
inayohusiana na mziki, na
ilianzisha kituo cha radio cha
iTunes mwaka uliopita.
Apple kuinunua Beats kwa dola
bilioni 3
Ijapokuwa kampuni hiyo ya
Carlifornia ndio walikuwa
waanzilishi wa zamani wa mziki
wa mfumo wa dijitali, imekuwa
ikikumbwa na ushindani mkubwa
kutoka kwenye huduma
zinazolipiwa kama vile Spotify,
Pandora na Rdio.
Hata hivyo, huduma ya mziki ya
Beats ina wateja wapatao 110,000
pekee waliojisajili ikilinganishwa
na Spotify ilio na watu milioni 10
waliojisajiliwa.
Mkataba huo na kampuni ya
Beats imeonyesha kudidimia kwa
Apple ambayo hujulikana kwa
kutengeneza bidhaa mpya wala
sio kununua kampuni ndogo
ndogo kama wanavyofanya
wapinzani wao Google.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.