Breaking News
recent

Ford yaagiza magari milioni1 kurejeshwa

Magari zaidi ya milioni moja
yanahitilafu ya usukani
Kampuni kubwa ya kutengeza
magari nchini Marekani
imeagiza magari milioni 1.4
yarejeshwe kutokana na
hitilafu ya usukani.
Takriban magari milioni 1.1
yaliyoundwa kwa mtindo wa
kispoti yaliyokuwa yameuzwa
Marekani Kaskazini yametakiwa
kurejeshwa kwani huenda yana
hitilafu kwenye usukani.
Vilevile magari mengine 200,000
yenye muundo wa Taurus
yaliyoundwa kati ya mwaka wa
2010 na 2014 huenda
yakakumbwa na tatizo ya kushika
kutu kwa haraka.
Matukio kama hayo yaliyofanyika
majuzi huenda yakaifanya
kampuni hiyo kuvunja rekodi ya
kutaka magari mengi zaidi
yarejeshwe katika kipindi cha
mwaka mmoja.
Magari zaidi ya milioni moja
yanahitilafu ya usukani
Urejesho huo umetokea wakati
sakata ya usalama inawakumba
wapinzani wakuu wa kampuni ya
hiyo , General Motors (GM).
GM ililaumiwa kwa kutotoa ilani
za kiusalama kwamba baadhi ya
magari yake hata baada ya
kubaini kuwa magari hayo
yanazima ghafla.
Dosari hiyo imehusishwa na vifo
13, ingawa wasanifu wa Marekani
wanaamini kuwa idadi hiyo
itaongezeka.
Pindi tangazo hilo lilipofanywa,
kampuni za kutengeneza magari
hayo pamoja na wasanifu wa
Marekani wameongeza juhudi za
kurejesha magari ambayo
yanapatikana kuwa na dosari.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.