Breaking News
recent

Lazio: Minala ana miaka 17 sio 42

Lazio; Minala ana miaka 17 sio 42
Uchunguzi wa shirikisho la soka
la Italia umebaini kuwa
mchezaji tineja wa Cameroun
Joseph Minala ana umri wa
miaka 17 wala sio 42 kama
ilivyodhaniwa na kuripotiwa
katika vyombo vya habari.
Mnamo mwezi Februari mtandao
mmoja wa michezo barani Afrika
ulichapisha habari ambayo ilizua
dukuduku iwapo kiungo huyo
alikuwa amedanganya umri wake .
Mtandao huo ulichapisha habari
za kuashiria kuwa hakuwa tineja
bali mtu mwenye umri wa miaka
42.
Lazio; Minala ana miaka 17 sio 42
Uchunguzi uliofwatia ulimlazimu
kukatiza kwa muda mipango yake
ya kucheza soka ya kulipwa hadi
pale matokeo ya uchunguzi
yangewekwa wazi na maafisa wa
shirikisho la soka la Italia.
Minala alijiunga na klabu hiyo
yenye makao yake mjini Rome na
hata alishiriki mchuano wa vijana
wasiozidi umri wa miaka 23 wa
Viareggio mnamo mwezi wa
Februari.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.