Breaking News
recent

‘Men In Black’ bila Will Smith itakuaje, ni kweli Will Smith hatoigiza kwenye Men In Black 4!?


Kama vile ilivyo brand ya movie ya Bad Boys, movie za Men In Black haziwezi kuongelewa bila kumtaja staa wake Will Smith na kama ulikuwa hujui basi taarifa ikufikie kuwa part 4 ya movie hiyo iko njiani mtu wangu lakini bad news ni kwamba Will Smith hatokuepo kwenye movie hiyo safari hii, kwa nini!? iko hivi…
MIB
Will Smith na Tommy Lee Jones kwenye movie ya Men In Black 3 mwaka 2012.
Watengenezaji wa movie hiyo Walter Parkes na mwenzake Laurie MacDonald walipata time ya kukaa na kuongea na mtandao wa The Hollywood Reporter wa Marekani na kueleza kwanini wameamua kutokumuweka Will Smith kwenye movie hiyo safari hii..
>>> “Tunatengeneza kama series ya muendelezo wa movie iliyopita, tutaibadilisha kidogo na pengine Will Smith hatoonekana kwenye muendelezo wa movie ya safari hii… tuna mtazamo tofauti safari hii wa jinsi tunavyotaka kuipeleka brand ya Men In Black, Will Smith amefanya kazi nzuri sana kwa movie zilizopita ila safari hii tumesukumwa kufanya vitu tofauti kidogo…” <<< @Laurie MacDonald.
MIB2
Walter Parkes na mwenzake Laurie MacDonald watayarishaji wa movie za Men In Black.
Movie za Men In Black zimemuingizia Will Smith hela ndefu sana kwa miaka yote aliyokuwa anazicheza na licha ya yeye kutokuepo kwenye movie hiyo time hii, mwigizaji huyo ameungana na rapper Jay Z na pamoja wanategemea kutengeneza mini series itakayo onyeshwa HBO hivi karibuni.
MIB3
Will Smith & Jay Z.
Will Smith na kampuni yake ya Overbrook Entertainment pia wana mpango wa kutengeneza movie itakayofana na series ya ‘The Fresh Prince of Bel-Air’, series iliyompatia umaarufu mkubwa sana Will Smith miaka ya 90.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.