Breaking News
recent

Waliovamia nyumbani kwa Big sean na kupora kazi zake waliacha ujumbe wenye e-mail yao kama atazihitaji tena

Wiki iliyopita taarifa za kuvamiwa kwa nyumba ya Big Sean iliyopo Los Angeles, Marekani wakati akiwa mapumzikoni Dubai zilienea mtandaoni ambapo wezi waliovamia nyumbani hapo waliiba vitu vyenye thamani ya dolla 150,000 na kuondoka na nyimbo za rapper huyo ambazo hazijatoka.
Taarifa mpya zina sema wezi hao ambao wanadhaniwa kuwa watu wa karibu na rapper huyo waliacha ujumbe wenye e-mail yao iwapo Big sean atahitaji kurudishiwa nyimbo zake hizo.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa kesi hiyo kwasasa infatiliwa na kikosi maalumu  “special unit” cha LAPD
Imeripotiwa kuwa lengo la wezi hao kuacha ujumbe huo ni kwa ajili ya kutaka rapper huyo awalipe kiasi kikubwa cha pesa ili apate nyimbo zake na ripoti zingine zimedai kuwa ni mpango wa wezi hao kuwachanganya polisi kuwatafuta kupitia email hiyo isiyo ya kweli.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.