Breaking News
recent

Haya ni mambo yanayowezakukwamisha mafanikio yako bila mwenyewe kujua...

Kuna watu wakinunua gari mpya  wanaita mafanikio, wengine kununua au kujenga nyumba kwao ni mafanikio, kila mtu anatafakari mafanikio  vile yeye anavyoelewa, mi naelewa mafanikio ni kutoka sehemu moja kwenda nyingine kimaendeleo. Kufanikisha mambo yote ya msingi, kuwekeza na bado umeweka Akiba. Sitoshangaa kama wewe mafanikio yako ni kununua nguo mpya au kiatu kipya hayo yanaweza kuwa kwako mafanikio watu tunatofautiana sana kwenye kufikiri. Ila umeshawahi kuwaza kwanini hufanikiwi katika maisha Yako ?
Huna Malengo ya Baadae
Kuna watu hawajui ndoto zao,hawajui nini wanataka kufanya katika maisha yao, wapo walio na ndoto za kufanya mambo kadhaa kama kuwa wanamitindo, wanamuziki au wacheza filamu lakini hawajui wapi wanaanzia, unatakiwa kujua unaanza wapi, kuwa kiongozi wa maisha yako mwenyewe kwa kupanga mipango yako weka plan A na plan B na hakikisha unafanikisha, jiekee muda (Deadline) mfano ndani ya miaka 5 au zaidi uwe umefanikisha malengo hayo.
Una Marafiki ambayo sio mfano wa kuigwa
Unapohitaji maendeleo jaribu kuachana na marafiki ambao kazi yao kubwa ni kukukatisha tamaa au kukurudisha nyuma kimaendeleo, kutana na watu wenye fikra chanya (Positive People) kaa na watu ambao wana mchango mkubwa wa maendeleo yako.  Mchango sio lazima uwe pesa unaweza kuwa mawazo au mchongo.
Muoga wa kujaribu
Kuna kukosea sana wakati wa kuaanza chochote, usiogope kujaribu tena kama ulishindwa mara ya kwanza kila alie na mafanikio hakuanzia juu,wote walianzia chini, fanya unachopenda na sio unachoweza kufanya. Kufanya kazi kwa kuwa unaipenda utafanikiwa kuliko kufanya kazi sababu unaiweza.
Haukubali Makosa yako
Kubali kurekebishwa, hauwezi kuwa uko sahihi wakati wote, sote tunakosea ila kuna wakati wa kuruhusu watu wakukosoe pale unapokosea kwani ndo njia raisi ya mafanikio  na unatakiwa kujifunza kupitia makosa hayo kama biashara ilikufa mwanzo lazima ujue nini kilisababisha ikafa na usije ukafanya makosa kama hayo tena.
Huweki Akiba
Kuna watu wanadhani akiba lazima uwe na mamilioni  katika akaunti ya benki lakini kama unafikiria mbele zaidi lazima uwe na akiba kwa kila unachopata, au hata uwe umewekeza katika biashara hii itakusaidia kupata kipato zaidi ya kimoja. Biashara sio lazima ufungue kampuni watu wanaanzia chini. Kwenye pikipiki,Bajaj  Hadi  maroli ya kusafirisha mizigo usikate tamaa.
Unatumia kuliko unachopata
Starehe gharama sana wote tunajua, kuna usemi unasema “Work Hard Play Hard” fanya kwanza kazi kwa bidii, kuna watu wanapenda starehe hadi wanakopa pesa za kunywa pombe wanakuwa na madeni ambayo hayana faida, hiyo sio akili.
Unajifananisha na wengine
Kitu kimoja watu wengi hawajui Hamisi hawezi kuwa Nasibu acha tabia ya kujifananisha na mtu na kuwaza kwanini hujawa kama yeye, yeye ana njia zake za maisha tofauti na zako jaribu kutafuta vya kwako. Na usijaribu pia kugeza kupitia njia zake za maendeleo kama yeye anafanikiwa kwa kuuza viatu sio lazima na wewe uuze viatu.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.