Breaking News
recent

Umetimiza malengo yako ya mwaka 2015 ? Haya ni mambo ya kuzingatia ili uweze kufanikisha ya mwaka ujao.

Tukiwa na Siku chache kumaliza Mwaka, ni wakati wa kuangalia nini umefanya ndani ya mwaka mzima, nini umeingiza nini umepoteza ulipanga ndoa imefanikiwa? Ulipanga biashara imefanikiwa? na vingine vingi  lakini wakati unaangalia nini umepata nini umejifunza  ni wakati pia wa kuangalia mbele, zimebaki siku chache mwaka uishe una mipango gani na mwaka mpya, kuna vitu vinaweza kuwa muhimu kwako au kwa mwengine lakini nadhani kila mtu anatakiwa kuzingati kabla hajaanza mwaka mpya.
Jaribu Mambo Mapya/ Kubali Mabadiliko
Umefanya kitu kimoja kwa mwaka na zaidi na hauoni mafanikio badilika, jaribu kujifunza mambo mapya, fanya mabadiliko juu ya mtazamo wako juu ya maisha,biashara,mahusiano,elimu na mengine mengi, unatembelea sehemu hizo hizo kila siku, filamu hizo hizo, marafiki hao hao, ni wakati wa kukutana na watu wapya na ujifunze mambo tofauti hii itakuza uwezo wako wa kufikiri.
Kazi, kazi, Kazi
Nimerudia kuonyesha msisitizo, fanya kazi, ulichokifanya jana kukufikisha hapo ulipo  leo,hakiwezi kukufikisha unakoenda kesho unahitaji kazi zaidi kufika unakoenda kesho, ongeza juhudi katika kazi zako, kama ni masomo ongeza juhudi pia, unahitaji kujishughulisha kuendelea maendeleo hayaji kwa kukaa na kula bata kila siku, badilika.
Umejifunza Nini kutokana na Makosa yako
Umeshindwa kufikisha malengo uliyoweka mwaka jana juu ya mwaka huu je unadhani malengo hayo yatafanikiwa  mwaka unaokuja. Unajua ulikosea wapi? Unajua wapi unatakiwa kuanzia ni wakati wako wa kijibu maswali hayo, na ni wakati wa kuangalia nini kilisababisha ukashindwa kufanikisha malengo yako. Na unatakiwa kufanya nini kukabiliana na changamoto hizo ni wakati wa kujifunza kutokana na makosa yako.
 Karibisha Mawazo Chanya/ Yaliyopita Yamepita
Toa mawazo finyu juu ya maendeleo yako, karibisha mawazo mapya katika kila jambo, na uyaache mambo ya nyuma  yapite na uwe tayari kukutana na mambo mengine mbele yako, huwezi badilisha historia lakini unaweza kutengeneza mambo ya mbele yako.
 Usifanyiwe Maamuzi na Mtu
Kuna watu bado kila anachotaka kufanya anahitaji aambiwe na mtu, mpenzi au mzazi hatukatai wazazi muhimu ila kuwa na maamuzi yako binafsi,ndugu, marafiki na jamaa wana umuhimu kwako, cha muhimu ni kujua nini unataka kufanya na ufanye kwa moyo. Jaribu kujiamulia na uwe nahodha wa maisha yako mwenyewe. Jua wakati gani wa kusema ndio na wakati gani wa kusema  hapana
Kuna Tabia za Kuacha
Kuna baadhi ya tabia ambazo zinakukwamisha, ni muhimu ukaziacha kama, ulevi ya kupindukia, uhuni, matumizi ya sigara na mengine mengi , jijengee tabia za maendeleo kutana na watu wapya, soma vitabu, tembelea sehemu hujawahi kwenda, jifunze lugha mpya, jifunze kucheza ala yoyote ya mziki. Tabia chanya ni chachu ya maendeleo.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.