Breaking News
recent

Kama unataka kuwa milionea badilika ufwate mfumo huu wa maisha....

Ni furaha kila unapo pokea mshahara au ujira wowote baada ya kazi Fulani, lakini kila ukitazama idadi ya madeni yanayokusubiri unaweza kupata kichaa, kwani unaweza ukagawa pesa hiyo na usibaki na shilingi ama la unabaki na pesa ya nauli na chakula, lakini nini cha kufanya kujiongezea kipato, watu ambao ni mamilionea hufanya mambo haya yafwatayo.

Jipangie Bajeti na Mpango wa kifedha
Ili uendelee lazima ujue, unatumia nini unaingiza nini? hii itakusaidia pia katika akiba zako na itakusaidia kama utachukulia swala hilo kwa umakini, kama kuna bili za kulipa kila mwezi na lazima uziweke katika mtiririko mzuri wa malipo ili bajeti zako siziingiliane na akiba  zako wala matumizi yako binafsi.

Uwe na Vyazo Vingine Vya Kukuingizia Kipato
Hakikisha mshahara wako sio pesa pekee unayoitegemea, lazima utengeneza mifereji mingine ya kukuingizia kipato, fanya kazi mwenyewe kama bosi wa biashara yako au ofisi yako, uza bidhaa zako kwa mitandao ya kijamii, anza kujitangaza taratibu sio lazima uanze na mtaji mkubwa.  ukiwa na vyanzo vingi vya mapato ni rahisi kuweka akiba na kuwekeza.

Akiba,Akiba, Akiba weka Akiba
Watu walioendelea waliweka akiba, punguza vitu unavyofanya visivyo vya maana au visivyo na umuhimu, punguza kutoka sana na kutumia pesa kwa starehe, fanya mambo ya muhimu tu acha kununua vitu ambavyo hauvihitaji, anza kwa kuweka akiba ndogo, ukiweka akiba nyingi ndiyo utaweza kuwekeza zaidi. wasichana wengi wanatabia ya kununua vitu wasivyo vihitaji kama viatu vingi,Nguo,Mikoba na vifaa vya  Urembo. Jiwekee kiwango cha wastani kulingana na mahitaji yako.

Punguza Matumizi  
Watu wengi wakipata pesa kidogo wanakimbilia magari ya bei kubwa na kufanya manunuzi ya vitu vya gharama kama nguo,saa na viatu kwenye maduka maarufu mjini, lakini  kama ungetumia pesa kuwekeza katika mambo ya muhimu kama biashara lazima baadae ikulipe kuna usemi mmoja unasema “Buy the best Car but Own the Best House”  na usinunue kitu ambacho haukihitaji sababu tu ni bei rahisi,

Kutana na Watu wenye Utaalamu
Kutana na watu walio kuzidi ujuzi,utaalamu na Uzoefu katika Biashara au shughuli unayotaka kuifanya hii itakusaidia kujifunza vitu kutoka kwao tembelea mikutano mbalimbali ya wataalamu na masomo  mbalimbali ya muda mfupi kujiongezea utaalamu, jiunge na wafanya biashara au wajasiriamali walio endelea katika kujifunza mambo ya kuhifadhi fedha, kuweka akiba na kuwekeza katika biashara.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.