Breaking News
recent

Fuvu la Shakespeare huenda liliibiwa

Uchunguzi wa kisasa uliofanyiwa kaburi la mwandishi mashuhuri William Shakespeare umeonesha huenda fuvu la kichwa chake liliibiwa.
Ugunduzi huo unaonekana kutoa uzito kwa ripoti zilizochapishwa katika vyombo vya habari 1879, ambazo baadaye zilipuuziliwa mbali na kutajwa kuwa uvumi, kwamba kuna watu walioiba fuvu hilo mwaka 1794.
Kundi la watafiti lilitumia teknolojia inayoweza kupenya ardhini (GPR) kutazama ndani ya kaburi hilo katika kanisa la Holy Trinity, Stratford ambao ni uchunguzi wa kwanza wa kiakiolojia kufanyiwa kaburi hilo.
Teknolojia hiyo iliwawezesha kuangalia ndani ya kaburi hilo bila kulifungua.
Mwanakiolojia Kevin Colls kutoka chuo kikuu cha Staffordshire, aliyeongoza uchunguzi huo akishirikiana na mtaalamu mwingine Erica Utsi, amesema: "Tumeangalia alimozikwa Shakespeare na tukaona kuna kasoro pahala ambapo kichwa chake kinafaa kuwa na kuna taarifa zinazodokeza kwamba huenda wakati mmoja kuna mtu aliiba fuvu la kichwa cha Shakespeare.

"Hili linanishawishi sana kuamini kwamba fuvu lake haliko katika kanisa la Holy Trinity kamwe." 
 
Uchunguzi huo ulikuwa sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 400 tangu kifo cha Shakespeare.
Kaburi ambamo Shakespeare alizikwa mwaka 1616 limeandikwa onyo na kulaani mtu ambaye atathubutu kufungua kaburi lake.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.