Breaking News
recent

Wanajeshi wa Somalia wauawa kwa Bomu

Milipukoi imekuwa ikijitokeza mara
kwa mara nchini Somalia
Takriban wanajeshi watano na
afisa wa jeshi wameuawa
katika mlipuko wa bomu mjini
Mogadishu,nchini Somalia
mashuhuda wameeleza.
Mlipuko huo unaelezwa kutokea
wakati wanajeshi hao wakipata
malipo yao nje kidogo ya mji huo.
Sababu ya mlipuko huo
haijafahamika,majeruhi kadhaa
wamepelekwa hospitalini kwa
matibabu.
Wanamgambo wa kiislamu, al
Shabab walitimuliwa kwa nguvu
mjini Mogadishu mwaka 2011
lakini wameendelea kufanya
mashambulizi nchini humo
Kundi hilo lenye uhusiano na
kundi la kigaidi la al -Qaeda
linadhibiti maeneo kadhaa katikati
ya Somalia.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.