Breaking News
recent

Waasi waua watu 1000 Afrika ya Kati

Wanamgambo wa kundi la anti-
balaka, Jamhuri ya Afrika ya Kati
Takriban watu elfu moja
wameuawa na waasi wa zamani
nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
katika mapambano yaliyodumu
kwa siku mbili yaliyojitokeza
mwezi huu, makadirio haya
yanazidi yale ya Umoja wa
Mataifa. Shirika la Amnesty
International limesema.
Shirika hilo limesema kuwa
uhalifu wa kivita bado unaendelea
kufanyika nchini humo.
Wapiganaji hao ambao wengi wao
ni Waislamu walimuondoa
madarakani aliyekuwa rais wa
taifa hilo, Francois Bozize mwezi
March, hali iliyosababisha
mgogoro ndani ya jamii nchini
humo.
Kiongozi wa waasi Michel
Djotodia hivi sasa ni kiongozi wa
kwanza kutoka jamii ya Waislamu
anayeongoza taifa lenye Wakristo
wengi na ndiye kiongozi wa mpito
wa Jamhuri ya Afrika ya kati.
Katika ripoti hiyo, Amnesty
International imesema waasi wa
zamani wa Seleka waliwaua
takriban watu 1000 mjini Bangui,
kwa kile kinachoelezwa kuwa ni
kulipa kisasi dhidi ya wapiganaji
wa Kikristo wanaodaiwa
kuwashambulia waasi wa Kiislam.
Idadi ya waliopoteza maisha
imeelezwa kuongezeka kuliko ile
iliyotolewa na Umoja wa Mataifa
ambao ulisema watu 450
waliuawa mjini Bangui na wengine
150 sehemu nyingine nchini
humo.
Mashambulio hayo yamekuja
baada ya wanamgambo
wajulikanao kwa jina la anti-
balaka ambao walikuwa wakiingia
kila nyumba na kuwaua watu 60
wa jamii ya Kiislamu. Amnesty
International imeeleza.
Askari wa Ufaransa nchini Jamhuri
ya Afrika ya Kati
Mashambulio yaliyofanywa na
wanamgambo wa zamani wa
Seleka yamehusisha mauaji pia
uvamizi na uporaji katika nyumba
za raia,ambapo wanawake na
watoto kadhaa wameuawa.
Shirika hilo limesema kuwa raia
huuawa kila siku mjini Bangui,
ingawa kumekuwepo na vikosi vya
Ufaransa na Umoja wa Afrika,
Ufaransa ikiwa na askari 1,600
nchini humo.
Shirika la kutetea haki za
binadamu la Human Rights Watch
limesema wapiganaji wa Kikristo
walishambulia jamii ya kiislamu
kaskazini mwa mji wa Bossangoa
na kuwachinja watoto huku
wakiwashinikiza wazazi wao
kushuhudia mauaji hayo.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Rais
Djotodia aliiambia redio ya
Kifaransa kuwa yuko tayari
kuzungumza na viongozi wa
wanamgambo wa Kikristo ili
kutatua mzozo huo.
Kauli hiyo imekuja baada ya
Umoja wa Afrika kuidhinisha
kuongeza vikosi vyake na kufikia
askari 6,000.
Vikosi vya Umoja wa Afrika na vya
Ufaransa vinafanya jitihada za
kuwanyang'anya silaha
wanamgambo hao.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.