Wataalamu nchini Uingereza wanasema
wamevumbua teknolojia ya kusoma midomo ya watu ambayo inaweza kubaini
wanasema nini bila kusikia wanachosema.
Teknolojia hiyo inaweza kusaidia sana kufahamu watu wanaonaswa kwenye kamera za siri za CCTV wanasema nini.Wataalamu hao katika chuo kikuu cha East Anglia wanasema teknolojia hiyo inaweza kutumiwa kukabiliana na uhalifu na ugaidi.
Lakini pia inaweza kutumiwa na wanahabari wanaofuatilia habari za wasanii na watu mashuhuri.
Watu ambao wamekuwa wakitumiwa kujaribu kusoma midomo ya watu wamekuwa wakitatizika sana kutofautisha sauti kama vile P na B.
Lakini wanasayansi hao wanasema teknolojia hiyo mpya inaweza kutofautisha sauti hizo.
Wataalamu hao wanasema pia kwamba teknolojia hiyo mpya itasaidia sana katika mifumo ya kukusanya habari kwa kutumia kompyuta.
No comments:
Post a Comment