Idara ya Haki ya Marekani imesema
huenda shirika la upelelezi la FBI limegundua njia ya kufungua simu ya
mkononi ya muuaji aliyewapiga risasi watu eneo la San Bernardino, Syed
Rizwan Farook.
Idara hiyo imeiomba mahakama kuahirisha kusikilizwa
kwa kesi kati ya shirika hilo dhidi ya kampuni ya utengenezaji wa simu,
Apple.Idara hiyo imekuwa ikishawishi mahakama ilazimishe Apple kufungua simu ya Farook, ambaye yeye na mkewe wanatuhumiwa kufanya shambulizi la bunduki na kuwaua zaidi ya watu 14 katika jimbo la California, Desemba, mwaka jana.
No comments:
Post a Comment