Rais Barack Obama akizungumzia
hali ya vita nchini Ukraine akiwa
Ikulu ya White House.
Ikulu ya White House imeeleza
masikitiko yake kuhusiana na
wapiganaji waasi wanaoungwa
mkono na Urusi Mashariki mwa
Ukraine kuwa wanatumia silaha
kubwa katika makabiliano
nchini humo.
Taarifa hiyo imetolewa mapema
Alhamisi baada ya helikopita ya
kijeshi ya Ukraine kudunguliwa na
bunduki kubwa ya kuangusha
ndege za kurusha makombora
ambapo wanajeshi 12 walifariki.
Na Rais Mteule wa Ukraine Petro
Poroshenko ameapa kuwaadhibu
"majangili" baada ya waasi
wanaoungwa mkono na Urusi
kuangusha helikopta ya kijeshi na
kuwaua watu 12.
"vitendo hivi vya uhalifu vya
maadui wa watu wa Ukraine
havitapita bila kuadhibiwa mtu,"
alinukuliwa kusema na shirika la
habari la Unian.
Helikopta ilidunguliwa karibu na
jiji la Mashariki la Sloviansk.
Jemedari mmoja alikuwa
miongoni mwa waliouliwa.
Kumekuwa na mapigano makali
kati ya waasi na wanajeshi wa
Ukraine katika Slovianski.
"Leo vijana wetu waliuawa
kikatili," Bwana Poroshenko
alisema Alhamisi.
"Huu ni wakati wa masikitiko
makubwa na nawatumia risala
zangu za dhati familia na jamaa za
wote waliopoteza maisha yao."
Urusi imekariri wito wake kuwa
Ukraine inapaswa kusitisha
kampeni zake za kijeshi dhidi ya
waasi wanaoungwa mkono na
Urusi ili "kuanzisha mashauriano
kamili ya kitaifa."
Katika tukio tofauti, Ukraine,
Urusi na Ulaya zinatazamiwa
kuanzisha awamu mpya ya
mashauriano mjini Berlin ambako
watajadiliana juu ya mzozo
unaohusu usambazaji wa gesi ya
kutoka Urusi nchini Ukraine.
Kampuni ya gesi ya Urusi
ijulikanayo kama Gazprom
imeisha kukatisha gesi
inayoelekea Ukraine iwapo
haitalipa deni kubwa linalokabili
taifa hilo.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment